Mshambulizi wa Arsenal, Alexis Sanchez. Picha/Getty Images
Mshambulizi wa Arsenal, Alexis Sanchez. Picha/Getty Images
Mkufunzi wa Arsene Wenger amefichua kuwa nyota wake ambaye hajatulia kimawazo Alexis Sanchez huenda akarejea dimbani kwenye mechi ya Jumapili hii dhidi ya Liverpool,kuwinda ligi kuu soka Uingereza EPL.

Sanchez ako na mwaka mmoja pekee kumaliza kandarasi yake na miamba hao na yu makini sana kuigura timu hiyo.

Aidha huenda atatoka kama mwanasoka huru mwishoni mwa msimu endapo hakuna dili yoyote kutoka kwa Man City na Chelsea ila kocha Wenger amesisitiza mwanasoka wake hapigwi bei.

Raia huyo wa Chile ameisakatia the gunners mara 103 huku akicheka na wavu mara 53 tangu aigure Bracelona mwaka wa 2014 kwenye dirisha la uhamisho.

Post a Comment

Previous Post Next Post