Mwanatenisi shupavu, Maria Sharapova akishiriki moja wapo ya mechi zake za ushindani. Picha/Getty Images
Aliyekuwa mwanatenisi nambari wani ulimwenguni Maria Sharapova alirejea kwa kishindo kwenye mashindano ya Grand Slam jumatatu 28 Agosti baada ya kibano alichopokea cha miezi 15 kutokana na kesi ya kutumia pufia, ni kutokana na mechi kati yake na mwanatenisi namba mbili ulimwenguni Simona Halep 6-4, 4-6, 6-3 kwenye makala ya US Open.Mwanatenisi huyo kutoka Urusi,mwenye umri wa miaka 30, alipata muda mgumu katika kurudia hali yake ya kawaida kutokana na jeraha ugani Arthur Ashe, baada ya ushindi wake mara 60 na kukosa ushindi kwa mara 64.


Akizungumza kuhusu ushindi wake, Sharapova anasema hakuamini macho yake kwa kuutua ushindi huo.
Kwenye ushindi huu, niliichukulia leo kama siku ya kawaida tuu, ila huu kwangu ni mwamko wa aina yake. Alisema Sharapova kwa furaha.
Huwa ninachukua muda mwingi kufikiria jinsi najitia nguvu na kufanya bidii kwenye kazi zangu, na leo ndio nimegudua ni kwa nini. Aliongeza Sharapova.   

Mshindi huyo mara tano ndani ya uchanjaa wa kimataifa wa Grand Slam, aliwapungia mashabiki mikono huku akipaza sauti yake kwenye kinasa sauti na kusema yeye ni msichana mwenye uchu na haendi popote, akiwa na maana kuwa yu ngali mchezoni.Sharapova alinaswa na chembe chembe za dawa za kutitimua misuli mwilini mwaka jana kwenye makala ya Australian open hali iliyo msababishia kukosa mashindano kadhaa na kumrudisha nyuma kwenye jedwali la wanatenisi bora Ulimwenguni.


Kwenye mchezo aliopiga Ugani hapo, alimshinda mpinzani hasimu mwenye miaka 25, raia wa Romania kwa jina Halep kwa kibano cha pointi zake 7-0.


Sharapova   alionekana mwenye wingi wa hisia. Akiwa anapiga hoi hoi na kuruka ruka juu kama kijitoto huku ameyafumba macho yake kwa furaha, yote haya akiyafanya kwa kusherehekea ushindi wake.

Baada ya hapo alimsalimia mpinzani wake Halep kisha akafunguka kwa mashabiki wake, 
Asanteni sana mashabiki wangu, kwa kunitia moyo kwenye Mchezo ambao umedumu kwa dakika 25.


Ukiwa mchezaji huwa hujui kile ambacho kinaenda kutokea kama ikiwa utashinda mchezo ama utaambulia patupu, yote ni hadi kipenga cha mwisho. 
Nafurahia sana utu mlio nao wa kunipa moyo. Alisaili Sharapova huku akibubujikwa na machozi ya furaha.


Sharapova alishinda mara 5 kati ya 22 alizocheza huku Halep akashinda mara 4 kati ya 10 kwenye mipambano ambayo imeshindwa na washindi 15.Hii ilikuwa mechi ya kwanza kwa Sharapova ugani Gran Slam, baada ya yeye kushindwa ugani humo kwenye awamu ya robo fainali na Serena Williams kwenye makala ya mwaka jana ya Australian Open.


Sharapova ambaye baadhi ya mataji aliyoshinda yanajumuisha taji la US Open aliloshinda mwaka 2006, mara hii atakuwa akipambana na Timea Babos kutoka Hungary ambaye hajawahi kukutana naye kwenye mpambano. 


Mrusi huyo anayeorodheshwa wa 146, alijaribu kurejea mchezoni Aprili ila kibano cha French Open kikawa kikwazo kwake, hali iliyomkosesha kushiriki makala ya Wimledon sawa na jeraha lililokuwa linamkabili.


Alipoulizwa kuhusu mapungufu yake, sharapova alihoji kuwa kuna changamoto za kila mtu, ila huo haukuwa muda mwafaka kwake kulizungumzia hilo.


Hata hivyo alimalizia kwa kusema kuwa anahitaji mechi kadhaa ilikurejelea mfumo wake awa kawaida aliokuwa nao hapo nyuma kabla hajapewa kibano.

Uandishi zaidi kutoka kwa Simon Ngaira

Post a Comment

Previous Post Next Post