Marcos Roho (kulia) na beki Ander Herrer (kushoto) wakiwa mazoezini August 22.Picha kwa hisani ya Getty Images
Marcos Roho (kulia) na beki Ander Herrer (kushoto) wakiwa mazoezini August 22.Picha kwa hisani ya Getty Images
Kiungo wa timu ya Manchester United inayoshiriki ligi kuu soka Uingereza EPL, amerejea kwenye kambi ya mazoezi mapema leo, hii ni baada ya kuwa mkekani kuanzia mwezi Aprili kutokana na jeraha la goti alilopata kwenye mechi ya kufuzu kwa taji la Uropa dhidi ya Anderlecht.  

Rojo anarejea kipindi ambapo meneja mkuu Jose Mourinho yu mbioni kukikita kikosi chake katika usasi wa taji la EPL msimu huu wa mwaka wa  2017-2018, huku akiwa amewasajili vifaa vizito kama  Nemanja Matic kutokea Chelsea na Romelo Lukaku aliyetwaliwa kutoka Everton. Ambao hadi sasa wametia natija.

Rojo ameonekana akiwa mchangamfu leo kwenye hafla ya mazoezi, huku akifanya mzaha na beki wa timu ya taifa ya Argentina na Man United Ander Herrera, akiwa anajaribu kuuziba uso wake kwa kipande cha kofia ya bushuti lake.

Hata hivyo, huenda Rojo akachukua muda mwingi nje ya uwanja ili kurejelea mfumo wake wa kawaida ili kocha wake raia wa Ureno amjumuishe kwenye kikosi cha kwanza msimu huu.

Hapo awali Morinho alidai kuwa huenda Rojo hangeweza kuonekana uwanjani hadi mwezi Desemba, na hilo labda laweza kuwa vigumu kumtia mbonini akiwa ugani hivi karibuni.

Miamba hao wa Old Trafford waliopata ushindi mnono wa magoli 4-0 wikendi iliyopita, watakuwa nyumbani O.T Jumamosi hii kuwavaa mabingwa wa msimu wa 2015-2016, Leicester City.

Maelezo zaidi kutoka kwa - Simon Ngaira

Post a Comment

Previous Post Next Post