Wachezaji wa SPEDAG wakiwa mazoezini. Picha/Kwa hisani
Wachezaji wa SPEDAG wakiwa mazoezini. Picha/Kwa hisani
Ligi kuu ya akina dada nchini inarejea wikendi hii baada ya kupiga breki kwa muda wa mwezi mmoja kufungua dirisha la uhamisho.
Katika zoni A, Soccer Queens itawaandaa Kayole Starlets katika uga wa Impala saa tano Jumamosi  huku  Soccer Sisters ikigaragazana na Mathare United Women kwenye mechi ya pili majira ya saa saba adhuhuri.
Mnamo Jumapili Mombasa Olympic itamenyana na Spedag uwanjani Mbaraki Mombasa kuanzia saa tisa alasiri.
Wakati huo huo kwenye zoni B, viongozi Vihiga Queens watasafiri hadi Busia kuwavaa Bulemia Jumamosi saa saba, kisha Jumapili ishuhudie Palos Ladies ikiwa nyumbani kucheza na Oserian Ladies katika uchanjaa wa Moi Kisumu huku Wadadia wakigaragazana na Vihiga Leeds katika uga wa  Mumias Sports Complex.
Mechi moja aidha iliyoratibiwa kuhusisha Thika Queens na Makolanders Jumamosi hii imehairishwa hadi itakapotangazwa tena.
Ligi ya daraja la kwanza kwa akina dada pia itarejelewa huku mechi mbili zikipangwa kuandaliwa Jumapili kwenye zoni A na moja ya zoni B ichezwe Jumamosi.
Golden Angels itamenyanana Gaspo Youth katika uchanjaa wa  Ziwani huku JUTAM ikikabiliana na Kibera Girls Soccer Academy katika uga wa JKUAT.
Kwenye Zone B, Solasa Stima Queens itapepetana na Kendu Bay Starlets.


Post a Comment

Previous Post Next Post