Gareth Bale wa Real Madrid akisherehekea goli kwenye moja wapo ya mchezi za klabu yake.Picha/Getty Images
Gareth Bale wa Real Madrid akisherehekea goli kwenye moja wapo ya mchezi za klabu yake.Picha/Getty Images
Maneja wa miamba wa Uhispania Real Madrid, Zinedine Zidane amekanusha ripoti zinazozagaa kumhusu wing’a matata wa timu ya taifa ya Wells na klabu ya Real Madrid Gareth Bale kuwa huwenda ataigura timu hiyo na kurejea Uingereza, mara hii kwa klabu cha Manchester United kwa kitita cha Euro milioni 92 (£92m).  

Kulingana na Zidane ni kuwa, kulikuwepo na lalama kutoka kwa Bale, akiwalaumu mashabiki wa Bernabeu, ambao walimpigia kelele siku ya jumapili Usiku, timu yake ya Real ilipoandikisha sare ya 2-2 na Valencia kwenye mchezo wa ligi kuu ya La Liga, kitu ambacho kilimuudhi sana mchezaji huyo.

Kufikia leo, ripoti kwenye mitandao kule Uhispania zimedokeza kuwa huwenda Bale akahamia Manchester United, Hii ni kutokana na wasilisho la miamba hao wa Uingereza kutoa kitita cha £92m ili kumnasa.,

Kocha Zidane amekanusha na kusema kuwa hayupo tayari kumuachia Bale kwenda popote na kuwa angali anamhitaji ugani Santiago Barnabeu.

Gareth ni Gareth tu, ni moja wapo ya wachezaji nilio nao wazuri. Tunafanya kila bidii na yote haya tunategemea pakubwa mchango wake jinsi ilivyo kwa wachezaji wengine maana kichango ni kuchangizana. 

Naeza sema amekuwa na ufungaji mzuri wa magoli, ila kwa sasa idadi hiyo imeanza kurudi chini na tunafanya kila mbinu kumrudisha kwenye mchezo wake wa kawaida.

 Kwa hivyo siwezi nikasema kuwa kuna mchezaji anayechukiwa ama tusiyempenda, kila mchezaji ana umuhimu kwenye kikosi changu, na hilo ndilo hunipa furaha siku zote nikiona ushirikiano wao na kwa maana hiyo Bale sitamwachilia.” Alisema Zidane.

Kwenye mchezo huo ambao Real ilidondosha alama kwa sare ya 2-2  na Valencia, Bale alionekana kuzibwa kwa kivuli cha wing’a wa kushoto kinda Marco Asensio, ambaye alichana wavu mara mbili, ikizingatiwa kuwa alicheza bembezoni kushoto mwa uwanja, Karim Benzema katikati huku Bale akipiga kwenye chaki za kulia bila mafanikio ya kufunga japo goli moja.

Ripoti zaidi kutoka kwa – Simon Ngaira.
 

Post a Comment

Previous Post Next Post