Philippe Coutinho. Picha/Getty Images
Philippe Coutinho. Picha/Getty Images

Klabu ya Barcelona imeripotiwa kutekeleza ofa ya mwisho kwa wing’a wa Liverpool Philippe Coutinho.

Tetezi zisizodhibitishwa zinaarifu kwamba miamba hao wa Uhispania wametia saini mkataba wa pauni milioni 138 sawa na Euro milioni  101 ada ya uhamisho pamoja na pauni milioni 37 kama nyongeza ili kuwafanya  The Reds kuachilia kifaa hicho au wakate tamaa.

Coutinho, ambaye hajacheza kwenye kikosi cha kocha Jurgen Klopp msimu huu kutokana na jeraha la mgongo anasemekana kuwa makini kuelekea ugani Camp Nou kwa mkataba wa miaka mitano.


Klopp kwa upande wake ameshikilia kuwa mbrazi, huyo hatapigwa bei.

Post a Comment

Previous Post Next Post