Mwanariadha Wilson Kipsang. Picha/ Getty Images
Mwanariadha Wilson Kipsang. Picha/ Getty Images

Kenenisa Bekele atajiunga na Wakenya Eliud Kipchoge na Wilson Kipsang kwenye mtimko wa BMW Berlin Marathon mnamo Septemba 24 kama jinsi ilivyotangazwa na waandalizi.


Kujumuishwa kwa Bekele ambaye ni mwanariadha wa pili mwenye kasi zaidi katika mbio za Marathon kwa wakati wote, kunaibua upinzani mkali na msisimko wa hali ya juu katika mbio hizo zinazojuisha wanariadha watatu kati ya watano wa kwanza orodhani katika fani ya wanaume.


Kipchoge anafukuzia kuvunja rekodi ya ulimwengu iliyonakiliwa na Mkenya mwenake Dennis Kimetto jijini Berlin mwaka wa 2014.
Dennis Kimetto akiwa katika kilomita 40 eneo la Gendarmenmarkt alipovunja rekodi ya dunia ya Marathon jijini Berlin,mwaka wa 2014. Picha/Kirsten Kortebein
Dennis Kimetto akiwa katika kilomita 40 eneo la Gendarmenmarkt alipovunja rekodi ya dunia ya Marathon jijini Berlin,mwaka wa 2014. Picha/Kirsten Kortebein
Aliweka dalili za kuafikia hilo mwezi Mei, alipotimka muda wa saa 2:00:25, muda wa kazi zaidi kushuhudiwa katika masafa marefu, kwenye msururu wa mjini Monza, Italy.


Ufanisi huo aidha ulifanikishwa kwa usaidizi wa wanariadha wanaochochea kasi (pacemakers), walioanza janja janja zao tangu mwanzo wa mbio.


Katika mbio za kawaida, wachochea kasi watatu ndio huruhusiwa na hawawezi kubadilishwa na wengine mbio zikiendelea.
Mjini Monza nilikuwa karibu kuvunja rekodi ya saa mbili. Alisema Kipchoge.


Mtimko wa Berlin unanipa nafasi mwafaka ya kuwinda kuvunja rekodi ya dunia.

Akiwa na miaka 32, Kipchoge anaweza kukadiria ufanisi wa taaluma yake kama mwanariadha wa masafa marefu.

Alishinda taji la mita 5000 mwaka wa 2003, sawa na medali za fedha na shaba kwenye mashindano ya olimpiki mbio zizo hizo mwaka wa 2004 na 2008 mtawalia, na ni bingwa mtetezi wa ubingwa wa olimpiki mwaka jana jijini Rio.


Wakati uo huo, mawio mema kwa mwanariadha mwengine wa nyumbani mwenye miaka 35 Kipsang yalijiri kwenye makala ya 40 ya mbio hizo alipoikosa rekodi ya dunia kwa tofauti ya sekunde 15, ni rekodi ya saa 2:03:38 iliyoandikishwa na Mkenya mwenzake Patrick Makau.

Rekodi ya dunia ya Kipsang ya saa 2:03:23 ilidumu kwa miezi 12 pekee kwani mwaka wa 2014 Kimetto aliibuka mwanaume wa kwanza kutimka Marathon chini ya muda wa saa 2:03 na kuandikisha jumla ya muda wa saa 2:02:57 kwenye mtimko wa Berling, rekodi inayosalia hadi sasa.


Mwaka jana jijini Berlin, Kipsang alitimka kasi ya sekunde kumi kushinda rekodi yake ya dunia ila amaliza wa pili nyuma ya Bekele. Mhabeshi huyo alinakili muda bora wa kibinafsi wa saa 2:03:03, zikiwa ni sekunde 6 pekee nje ya rekodi ya dunia.


Kipsang alinga’nga’na katika nusu ya mbio hizo ila hakuwa na nguvu za kumfikia Bekele zikisazwa kilomita mbili.


Mbio za mwaka jana zilimwacha Kipsang na imani kuwa miguu yake ina kasi zaidi, kitu anachotaka kukidhihirisha mwezi ujao.

Ninatiwa nguvu zaidi na mazoezi niliyofanya na naweza kusema nipo tayari kushinda siku zingine zote. Aliweka sawa Kipsang.


Bekele aliweka historia ya kuwa mwanariadha wa pili mwenye kasi zaidi duniani licha ya kuvuna majeraha ya msuli mara nyingi kwenye nusu ya mbio hizo ila alijikakamua kumaliza na ufanisi.
Mwanariadha wa Ethiopia, Kenenisa Bekele. Picha/Getty Images
Mwanariadha wa Ethiopia, Kenenisa Bekele. Picha/Getty Images
Bekele mwenye miaka 35, ni mwariadha mfanisi zaidi katika mbio za masafa marefu kwenye historia.

Ni Bingwa mara tatu wa olimpii na bingwa mara tano wa dunia katika mita 5000 na 10,000. Pia ameshinda mataji 11 ya world cross country katika msafa yote, marefu na mafupi.
Kiujumla,  bingwa huyo anashikilia ubingwa wa dunia wa mita 5000 na 10000.


Post a Comment

Previous Post Next Post