Katika pite pite zangu kama muandishi kwenye mishemishe za kutafuta maisha kupitia uandishi, kalamu yangu imevuka boda hadi mjini njombe Tanzania. Kisha leo imekita kambi ndani ya kituo cha redio kilichopo hapa Njombe maarufu kama ICE 99.5 FM. Japo wanahabari hapa ndani niwengi ila kwa leo nataka kumuangazia mwandishi na mtangazaji wa habari za burudani kwenye kipindi maarufu cha Zero Planet. Ambacho huwa kina ruka kila siku ya wiki kwanzia Jumatatu hadi Ijumaa na kaka yetu Gami Dee. Gami pia huwa anaongoza vipindi tofauti kupitia redio hii ya ICE FM ikiwemo kipindi cha ClubIce na Top 20.

Gami Dee| Photo| By Changez Ndzai

Gami Dee| Photo| By Changez Ndzai

Sasa inawezekanaje mtu mmoja kufanya kazi hizi zote kwa wakati mmoja? Hii inamaanisha bidii na hekima ni kitu cha ziada kinachomuezesha star huyu kuyafanya haya kwa wakati mmoja. Na nikutokana na juhudi zake hizi, ndipo limuko la riwaza yetu ya (EaBana) imemuangazia kwa kina. Mbali nakuwa mtangazaji hapa, nimesema hapo awali kuwa jamaa huyu ni pia huwa ni muandishi. Na kazi zake za uandishi zimekuwa zikizikonga nyoyo za mashabiki wa tovuti za habari ikiwemo Bongo5. Pengine kufikia hapo unaweza kuwa umeipata picha kamili ya star wetu wa leo Gami Dee, pia kabla sijafunga ukurasa huu, licha ya kutubariki na habari za burudani ni mmoja wa wadau wanao peana msukumo wa nguvu katika kuhakikisha wasanii wa Bongo wanafanikisha malengo yao. Nahii imemupelekea yeye kuja na tuzo zake mwenyewe za burudani (Nyota Awards), ambazo waimbaji wa kutoka mkoa wa Njombe walihusika vilivyo. Hebu burudika na baadhi ya picha na kazi zake kupitia vishikanishi hivi vya mtandao wake wa YouTube. Burudika!


Gami Dee| Photo| By Changez Ndzai

Gami Dee Akiwa kwenye mishemishe zake The Dock| Photo| By Changez Ndzai


Gami Dee| Photo| By Changez Ndzai

Gami Dee kwenye kipindi cha Zero Planet| Photo| By Changez Ndzai


Sikiliza baadhi ya kazi ya Gami hapa akiwa studioni
Gami Dee| Photo| By Changez Ndzai

Gami Dee Akiwa na Mbunge kwenye studio| Photo| By Changez Ndzai


Post a Comment

Previous Post Next Post