Droo ya makundi ya ligi ya mabingwa Uropa ikiandaliwa Monaco 24/08/2017. Picha/Getty Images
Droo ya makundi ya ligi ya mabingwa Uropa ikiandaliwa Monaco 24/08/2017. Picha/Getty Images
Klabu ya Tottenham Hotspurs imepangwa katika kundi la kufa kupona dhidi ya bingwa mtetezi Real Madrid, miamba wa soka Ujerumani Borussia Dortmund na Apoel Nicosia ya Cyprus, katika droo ya klabu bingwa barani Uropa iliyofanyika jana jioni.

Wenzao kutoka London na mabingwa wa ligi kuu soka nchini Uingereza Chelsea wamo katika chungu kimoja na Atletico Madrid, AS Roma ya Italia na FC Qarabag.

Manchester City waliomaliza wa tatu katika EPL msimu jana wamepangwa dhidi ya Napoli ya Italia, Shaktar Doneshk ya Ukraine na Fayenoord.

Manchester United walofuzu kwa kushibnda taji la Uropa League licha ya kumaliza nnje ya nne bora wamo katika kundi Monaco, Basel na CSKA Moscow.

Liverpool nao watavaana na  Benfica, Maribor na Spartak Moscow.DROO KAMILI YA MAKUNDI;

KUNDI A:
Benfica
Manchester United
Basel
CSKA Moscow

KUNDI B:
Bayern Munich
Paris St-Germain
Anderlecht
Celtic


KUNDI C:
Chelsea
Atletico Madrid
Roma
Qarabag

KUNDI D:
Juventus,
Barcelona
Olympiakos,
Sporting

KUNDI E:
Spartak Moscow
Sevilla
Liverpool
Maribor

KUNDI F:
Shakhtar Donetsk
Manchester City
Napoli
Feyenoord

KUNDI G:
Monaco
Porto
Besiktas
RB Leipzig

KUNDI H:
Real Madrid
Borussia Dortmund
Tottenham
APOEL


Post a Comment

Previous Post Next Post