Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akisherehekea goli la pili na wenzake timuni lililoipa klabu yake ushindi wa 2-1 dhidi ya Fiorentina kwneye mechi ya kombe la Santiago Bernabeu tarehe 23/08/2017. Picha/Getty Images
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid akisherehekea goli la pili na wenzake timuni lililoipa klabu yake ushindi wa 2-1 dhidi ya Fiorentina kwneye mechi ya kombe la Santiago Bernabeu tarehe 23/08/2017. Picha/Getty Images
Mchezaji bora ulimwenguni na mshambulizi wa timu ya Ureno na klabu ya Real Madrid Cristiano Ronaldo aliisaidia klabu yake ya Real kutwaa kombe la Santiago Bernabeu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fiorentina uwanjani Santiago Bernabeu.

Christiano analiyezabwa kibano cha kuzuiliwa kucheza mechi tano za ligi ya La Liga msimu huu,sawa na kesi inayomwandama ya kutolipa kodi iliyowasilishwa mahakamani dhidi yake, aliyaweka hayo yote kando usiku wa hapo jana na kuisaidia timu yake kuvuna ushindi wa Kombe la Santiago kutoka kwa  Fiorentina.

Kombe hilo lilikuwa  la kusherehekea ukumbusho wa miaka 60 tangu kuangamaia kwa wadau wa timu hiyo kwenye ajali ya ndege ndege iliyowaua watu wengi uwanjani Santiago mwaka wa 1957 kwenye fainali za kombe la Uropa.

Mchezaji huyo mwenye miaka 32, alifungua safu ya magoli dakika za kwanza kwanza za mchezo kwa bao lake la kwanza ambalo baadae lilisawazishwa na Jordan Veretout wa Fiorentina, kabla ya kukiramba kimia tena na kufanya mambo kuishia 2-1.

Hata hivyo kumekuwa na tetesi kuwa huwenda Cristiano anaweza kuigura Madrid na kurejea kwa klabu yake ya zamani ya Manchester United nchini Uingereza. Inasemekana kuwa uhamisho wake unahusu pakubwa misukosuko inayomkabili nchini Uhispania.

Kwa sasa Ronaldo amebakisha mchezo mmoja tu kati ya marufuku aliyopewa ya kutocheza mechi tano za La Liga baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu alipomsukuma mwamuzi kwenye mechi ya ufunguzi wa msimu maarufu “Spanish Super Cup” waliocheza dhidi ya mahasimu wao Barcelona.
 Hii ilikuwa ni mechi ya kwanza kwa Ronaldo kucheza msimu huu maana haipo kati ya zile tano alizopigwa marufuku.

Maelezo zaidi kutoka kwa Simon Ngaira

Post a Comment

Previous Post Next Post