Meddie Kagere wa Gor Mahia (Kulia)  akisherehekea goli pamoja na mwenzake Jacques Tuyisenge. Picha/www.sportpicha.co.ke
Meddie Kagere wa Gor Mahia (Kulia)  akisherehekea goli pamoja na mwenzake Jacques Tuyisenge. Picha/www.sportpicha.co.ke
Makosa mawili yaliyofanywa na manahodha wa Gor Mahia na Afc Leopads yalichangia magoli, debi la msehemeji lilipoishia sare ya 1-1 hapo jana jioni, ikiwa ni mechi ya mwisho ya ligi kuu soka taifa Kenya KPL ikisakatwa kwenye uga huo mwaka huu.

Nahodha wa Gor Musa Mohammed alijifunga dakika ya 19 katika harakati za kuuondosha mpira uliofyatuliwa na Sammy Ndung’u katika wing’a ya kulia ya Ingwee ila dakika ya 36 ila nahodha wa Leopards Robinson Kamura akarejesha tabasamu kwa nyuso za mashabiki wa Gor kwa kumpa Meddie Kagere wakati rahisi wa kukiramba kimia.

Kogalo sasa wanasalia kileleni mwa jedwali kwa tofauti ya alama sita wakiwa na mechi moja mkononi huku Leopards wakisalia kwenye nafasi ya 13, alama 20 nyuma ya Gor.
Mchezo ulikuwa mzuri, niliona vijana waling’ang’ana ,hii mechi tulikuwa tumeshinda ila tukafanya makosa sisi wenyewe lakini hatuwezi sema ni mbaya kwa kuwa tumevuna alama angalau moja.
Kuna muda Kogalo ilikuwa ikiilaza Ingwee wakati wowote ule ila leo tumefanya jambo kubwa sana kuwazuia.
Makosa makubwa ni yale ya beki Musa badala aondoshe mpira akataka kupiga chenga na mpira ukachukuliwa kisha ukatiwa kimiani.
Hiyo tumesahau kwa sasa tunaganga mechi ijayo. Swala langu la kudumisha nidhamu katika timu hii umeona jinsi lilivyopokelewa na wachezaji, leo wamedumisha nidhamu ya hali ya juu.Alisema kocha wa AFC LeOpards Robert Matano.
Mechi imekuwa ngumu sana ila tumejaribu sana kupata alama, kwa sasa tunangoja hiyo mechi nyingine kisha tuone vile kutakuwa.
AFC si timu rahisi ila tutajikaza tu kwa kila mechi tuone tunanusuru alama.” Alizungumza mwanasoka wa Gor, George ‘Blackberry’ Odhiambo.
Kocha wa AFC Leopards Robert Matano akiwaelekeza wachezaji wake kwenye moja wapo ya mechi ya ligi kuu KPL. Picha/Stafford Ondego, www.sportpicha.co.ke
Kocha wa AFC Leopards Robert Matano akiwaelekeza wachezaji wake kwenye moja wapo ya mechi ya ligi kuu KPL. Picha/Stafford Ondego, www.sportpicha.co.ke
Katika matokeo mengine Zoo Kericho waliipga Western Stima 4-1,Sony Sugar waakaandikisha sare tasa na Kariobangi Sharks, Kakamega Homeboys walisajili sare ya 1-1 na Tusker, huku Bandari wakipata sare japo ya 2-2 na Mathare United.

Gor Mahia ingali kileleni kwa alama 44 baada ya mechi 21 ikifuatiwa na Sofapaka iliyo ya pili kwa alama 38 baada ya kucheza mara 22, Posta Rangers ni ya tatu kwa pointi 35 baada ya mechi 22 huku Ulinzi na Kariobangi zikifunga safu ya tano bora kwa pointi 32 na 31 mtawalia ila wanajeshi wamejitosa ugani mara 20.
Post a Comment

Previous Post Next Post