Mashabiki wa Gor Mahia na Afc Leopards kwenye debi la awali la mashemeji ugani Nyayo
Mashabiki wa Gor Mahia na Afc Leopards kwenye debi la awali la mashemeji ugani Nyayo
Debi la mashemeji kuwinda ligi kuu soka taifa Kenya KPL baina ya Gor Mahia na Afc Leopards limerejeshwa tena uwanjani Nyayo na wala sio ugani Kasarani liliporatibiwa awali kutifua kivumbi.

Ngoma hiyo iliyokuwa ipigwe Agosti tarehe 27 ilikuwa isakatwe uwanjani Nyayo kabla ya kusukumwa Kasarani ila wakuu wa Kogalo wameomba ichezwe Nyayo kwani inasemekana uwanja wa Kasarani unaandaliwa kwa sherehe za kuapishwa kwa Rais.

Ni kweli kufikia sasa hatukuwa tumepata mwafaka wa uga wa Nyayo ila tumeongea na usimamizi wake na umeturuhusu kuutumia kwenye mehci yetu dhidi ya AFC Loepards Jumapili hii.alieleza naibu katibu mkuu wa Kogalo Rinald Ngala.

Mashabiki wengi hawakupendelea uga wa Kasarani unaobeba kiasi cha watazamaji  60,000 ikilinganishwa na Nyayo inayoingiza idadi nusu ya mashabiki hao.


Gor Mahia itapambana na Posta Rangers mnamo Agosti 23 uwanjani Kasarani kabla ya kushiriki debi hilo la Mashemeji.

Post a Comment

Previous Post Next Post