Kocha wa Harambee Stars Stanley Okumbi akiwajibika kwenye mechi ya ushindani.
Kocha wa Harambee Stars Stanley Okumbi akiwajibika kwenye mechi ya ushindani.

Aliyekuwa beki wa Gor Mahia Erick ‘Marcelo’ Ouma ametemwa nje ya kikosi kilichotajwa na kocha mkuu Stanley Okumbi hii leo.

Kipa mwenye tajriba Arnold Origi ameitwa tena kwenye kikosi cha timu ya taifa ya soka Harambee Stars kwa kibarua cha mechi za kirafiki.Origi amekuwa nje ya kikosi kwa zaidi ya mwaka mmoja na hivyo kuwashtua wengi kutokana na mwito wake.

Vigogo wengine timuni kama vile Michael Olunga, David ‘Calabar’ Owino na nahodha Victor Wanyama wamo kwenye listi hiyo ya wanasoka 15.

Kikosi hicho kinatarajiwa kukita kambi ya mazoezi Jumapili hii ya Agosti tarehe 27.

Kikosi kitakachoelekea Morocco kinatarajiwa kulimana na Mauritania na Togo Agosti tarehe 31 na Septemba 4 mwaka huu mtawalia kitaondoka Jumanne ya Agosti 29 huku timu itakayocheza na Msumbiji mnamo Septemba 2 ikielekea Maputo Agosti 31 mwaka huu.

ambapo kikosi kitakacholimana na  Morocco kinatarajiwa kumenyana na Mauritania na Togo Agosti tarehe 31 mwaka huu.

Kikosi kamili ni kama ifuatavyo.

Makipa

Boniface Oluoch (Gor Mahia)
Patrick Matasi (Posta Rangers)
Peter Odhiambo (Gor Mahia) 
Gabriel Andika (AFC Leopards)
Farouk Shikalo (Posta Rangers)Walinda ngome…

Benard Ochieng (Vihiga United)
Harun Shakava (Gor Mahia)
Musa Mohammed (Gor Mahia)
Simon Mbugua (Posta Rangers)
Collins Shivachi (Tusker)
Joseph Okumu (hana timu)
Jockins Atudo (Posta Rangers)
Robinson Kamura (AFC Leopards)
 Wesley Onguso (Sofapaka)
Dennis Shikhayi (AFC Leopards)
Na Pascal Ogweno (Kariobangi Sharks)


Viungo...

Ernest Wendo (Gor Mahia)
Victor Majid (AFC Leopards)
George Odhiambo (Gor Mahia)
Jackson Macharia (Tusker)
Alpha Onyango (Kakamega High School)
Duncan Otieno (AFC Leopards) 
Peter Nganga (Nakuru All Stars)
Kenneth Muguna (Gor Mahia)
Na Patillah Omotto (Kariobangi Sharks)


Washambulizi...

Boniface Muchiri (Tusker)
Kepha Aswani (Nakumatt)
 Masoud Juma (Kariobangi Sharks)
Boniface Omondi (Gor Mahia)
Moses Mudavadi (Kakamega Homeboyz)
James Mazembe (Kakamega High School)
Ezekiel Otuoma (Western Stima)
 Joe Waithera (Wazito)
Chris Ochieng (Mathare United)
Nicholas Kipkirui (Zoo Kericho)
na  Marcellus Ingotsi (AFC Leopards).


Wanasoka wenye makao nje ya nchi

Abud Omar (Slava Sofia, Bulgaria)
Anthony Akumu (Zesco, Zambia)
David Ochieng (New York Cosmos, Marekani)
Jesse Were (Zesco, Zambia)
Johanna Omollo (Cercle Brugge, Ubelgiji)
David Owino (Zesco, Zambia)
na Michael Olunga (Guizhou Zhicheng, China)

Wengine...

Clifton Miheso (Buildcon FC, Zambia)
Erick Johanna (Vasalund’s FC, Uswidi)
Mark Makwatta (Buildcon FC, Zambia)
Jonah Ayunga (Galway United, Ireland)
Brian Mandela (Maritzburg United, Afrika Kusini)
Ayub Timbe (Beijing Renhe, China)
Victor Wanyama (Tottenham Hotspurs, Uingereza)
na Arnold Origi (Lillestrom, Norway)Post a Comment

Previous Post Next Post