Mshambulizi wa Gor Mahia FC Meddie Kagere raia wa Rwanda akisherehekea goli na mwenzake timuni Timothy Otieno baada ya kutinga goli dhidi ya Nzoia United FC kwenye mechi ya ligi kuu KPL ugani  Mumias Sports complex, Kakamega mnamo Mei 14, 2017. Gor Mahia FC ilisajili ushindi wa bao 1-0 kwenye mehci hiyo. Picha/Stafford Ondego/www.sportpicha.com
Mshambulizi wa Gor Mahia FC Meddie Kagere raia wa Rwanda akisherehekea goli na mwenzake timuni Timothy Otieno baada ya kutinga goli dhidi ya Nzoia United FC kwenye mechi ya ligi kuu KPL ugani  Mumias Sports complex, Kakamega mnamo Mei 14, 2017. Gor Mahia FC ilisajili ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi hiyo. Picha/Stafford Ondego/www.sportpicha.com
Klabu ya Gor Mahia FC ilizidi kujithibitishia nafasi ya kunyanyua taji la ligi kuu soka taifa Kenya KPL kwa kuisaga Posta Rangers bao 1-0 hapo jana alasiri ugani kasarani.


Kogalo walipata bao hilo la pekee dakika ya 22 kupitia shuti lake Meddie Kagere aliyeunganisha krosi yake Keneth Muguna.

Kwenye uga uo huo, Sofapaka ilivuna ushindi wake wa pili na mabao manane katika mechi mbili walipoiwasha Nzoia 3-1 ambapo Umar Kasumba alifunga mawili na mwenzake Ezekiel Okare akafunga moja huku Nzoia ikifutwa machozi kupitia bao la Luke Namanda.

Western Stima kwa upande wake ilipokea kipigo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa vijana wapya ligini Kariobangi Sharks katika ngoma iliyochanjaliwa Kenyatta Machakos Stadium.

Mechi ilikuwa nzuri,tumecheza vyema tuliimarika katika idara zote.
Tulijipanga kuinuka zaidi katika kipindi cha kwanza jambo ambalo vijana wangu walilizingatia.
Siwezi kumlaumu mwamuzi  kwani mchezo maamuzi yake hayakuegemea upande wowote ila nimeangusha alama tatu na nitajizatiti kuona nimehsinda mechi ijayo” alisaili Henry Omino, fundi wa Western Stima.
Kutokea mehci nne mfululizo bila ushindi si mchezo.Tulikuwa tumekwenda sare mara mbili dhidi ya Homeboys  na Zoo kisha tukapoteza tena dhidi ya timu zizo hizo.
Nimefurahia sana kuvuna pointi tatu muhimu ambazo angalau zinatufikisha alama alama 30 katika nafasi ya tano.” Alinena kocha wa Sharks, William Muluya.
 Ugani Ruaraka, Mathare united isajili sare ya 1-1 dhidi ya Nakumatt ambapo Kepha Aswani alifungua chati za mabao kwa Nakumatt kabla ya mshambulizi Crispin Oduor kulirejesha goli hilo kupitia tuta la penanti.


Post a Comment

Previous Post Next Post