Wachezaji wa Senegal wakisikitika baada ya kusagwa 5-0 na Guinea iliyofuzu kushiriki kipute cha CHAN 2018 kitakachoandaliwa Kenya. Picha/Kwa hisani
Wachezaji wa Senegal wakisikitika baada ya kusagwa 5-0 na Guinea iliyofuzu kushiriki kipute cha CHAN 2018 kitakachoandaliwa Kenya. Picha/Kwa hisani
Amadou Sekou Camara alicheka na kimia mara tatu huku Guinea ikiiangusha Senegal mabao 5-0 hapo jana na kukamilisha orodha ya timu shiriki kwneye kipute cha CHAN mwaka ujao kitakachoandaliwa nchini Kenya.
Angola, Burkina Faso, Cameroon, Congo Brazzaville, Equatorial Guinea, Ivory Coast, Kenya, Libya, Mauritania, Morocco, Namibia, Nigeria, Sudan, Uganda na Zambia zilifuzu awali.

Guinea iliangukia kipigo cha 3-1 katika mkumbo wa kwanza yapata siku nane zilizopita na kuongoza mabao 3-0 kufikia kipindi cha mapumziko na hivyo kushinda kwa jumla ya mabao 6-3 matokeo ya mikondo yote licha ya kukosa mkwaju wa penanti jijini Conakry,mechi iliyocheleweshwa kwa saa 24 kutokana na mvua.


Kenya inatarajiwa kuandaa kipute cha CHAN kuanzia Januari tarehe 12 hadi Februari tarehe 4 mwaka ujao ila mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini FKF, Nick Mwendwa amehofia uandazi huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post