Rooney akisherehekea goli kwenye moja wapo ya mechi za timu ya taifa ya Uingereza. Picha/Getty Images
Rooney akisherehekea goli kwenye moja wapo ya mechi za timu ya taifa ya Uingereza. Picha/Getty Images
Mfungaji bora wa wakati wote wa timu ya taifa ya Uingereza Wayne Rooney amestaafu kutoka soka la kimataifa hii ni baada ya kukataa nafasi ya kuwa miongoni mwa kikosi cha Uingereza kwa mechi za mwezi ujao za kufuzu kwa kombe la dunia mwakani.

Rooney mwenye miaka 31 aliulizwa na kocha wake mkuu Gareth Southgate acheze kwenye mechi za Malta na Slovakia na badala yake akasema ni heshima na taadhima kuitwa kikosini ila ni wakati mzuri kwake yeye kustaafu soka na timu ya taifa.

Rooney amesema ni uamuzi mgumu ila aliuafikia baada ya kujadiliana na familia yake, meneja wake klabuni Everton na marafiki wake wa karibu.

Aidha aliongeza kuwa kuigura Manchester United na kujiunga na Everton pia ulikuwa uamuzi mzito ila amefurahikia kurejea nyumbani na sasa anataka kuwasaidia kunyanyua ligi kuu Uingereza msimu huu.


Rooney amesema atasalia kuwa shabiki wa three lions huku akijutia kutokuwa miongoni mwa timu ya taifa ya Uingereza iliyoshinda tajila ushindnai na amedai Wachezaji wanaojituma kama Gareth wanaweza kufuata nyayo zake na kuiletea timu mataji mengi.

Rooney hata hivyo amesema siku itawadia atakaporejea timuni humo kama shabiki au nafais nyingine.

Post a Comment

Previous Post Next Post