Wanasoka wa Harambee Starlets wakisherehekea moja wapo ya magoli 4 dhidi ya Burundi kwenye michuano ya CECAFA 2016 katika uga wa FUFA Technical center mjini  Njeru, Uganda, September 13, 2016. Harambee Starlets walishinda kwa mabao 4-0. Picha/www.sportpicha.com
Wanasoka wa Harambee Starlets wakisherehekea moja wapo ya magoli 4 dhidi ya Burundi kwenye michuano ya CECAFA 2016 katika uga wa FUFA Technical center mjini  Njeru, Uganda, September 13, 2016. Harambee Starlets walishinda kwa mabao 4-0. Picha/www.sportpicha.com

Timu ya taifa ya soka kwa akina dada Harambee Starlets inazidi kunogesha mazoezi yao katika uwanja wa Kasarani katika kujiandaa kwa makala ya mwaka huu ya kipute cha (COSAFA) kitakacho andaliwa jijini Bulawayo, Zimbabwe kuanzia Septemba 13 hadi 24 mwaka huu.
Kikosi ghafi cha wanaoska 30 na kocha wao mkuu Richard Kanyi akisaidiwa na Merry Odhiambo kilitua kambini kwenye uga wa kimataifa wa Moi Kasrani jumapili iliyopita, kikisubiriwa kutajwa kwa tarehe ya safari.
Akizungumza na meza yetu ya michezo, Rais wa shirikisho la soka nchini Nick Mwendwa, alihoji kuwa shirikisho hilo limejitolea kuipa timu hiyo ufadhili sawa na kusaidia timu hiyo kuzuru mataifa mengine kwa mechi mabali mbali za kimataifa ili kuwezesha timu hiyo kuwa maarufu kote barani Afrika na kimataifa.
Tunafaa kuwapeleka wasichana wetu kwa mechi kama hizi maana huwa zinasaidia kwenye makuzi mazuri ya vipaji na timu.
Baada ya kuwapeleka kwenye mashindano haya ya COSAFA, itakuwa ni rahisi kwetu kuzungumzia hatua ambazo tutakuwa tumepiga kwenye soka ya akina dada kwa ulimwengu,”
Hapo nyuma tulikuwa nyuma sana kwenye soka ya akina dada, ila kwa sasa ni moja wapo wa ajenda zetu kukuza soka ya akina dada jinsi inavyohitajika na Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA.
Tunafaa kuonesha ulimwengu hatua tunazopiga kwa soka ya akina dada, na hili ni moja wapo wa hatua hizo.” Alisema Mwendwa.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2016, Starlets ilicheza kwenye kombe la kimataifa la wanawake (AWCON), na kutokea hapo tumekuwa tukifuatilia kwa karibu timu hii yetu ya wanadada, kuanzia ile siku ya mashindano yaliyoandaliwa kule Cameroon.   
Wanadada wa Kenya watatifuana na wenzao wa Msumbiji kwenye mechi yao ya kwanza Septemba 14, na baadae waumize nyasi dhidi ya Mauritius Septemba 16. 
Baada ya hapo watahitimisha kampeni yao hiyo kwenye awamu ya makundi na wanadada wa Uswazi Septemba 18. Mechi hizi zote zitapigwa kwenye uchanjaa wa Luveve kule Zimbabwe.
Kufikia sasa ni timu za mataifa 12 kwenye makala hayo ya tano. Mataifa hayo ni , Lesotho, Botswana, Malawi, Kenya (waalikwa), Madagascar, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Uswazi, Zambia na mwisho kabisa Zimbabwe ambao ndio wenyeji.
 Zimbabwe itakuwa inaanda makala haya kwa mara ya tatu, baada ya kufanya hivyo mwaka wa 2002, 2011 ambapo walitua ushindi kwenye maandalizi hayo yote.
Viwanja vitatu vitatumika katika uandazi wa michezo hii, nayo ni Luveve, White City pamoja na Barbourfields  .
 Kikosi kizima cha Kenya;
Vivian Akinyi, Jenipher Adhiambo, Paul Atieno, Jane Achila, Wendy-Ann Achieng, Irene Awuor, Dorcas Shikobe, Caroline Anyango, Cheris Avilia, Sharon Bushenei, Mary Wanjiku, Dorcas Anyango, Jacky Ogol, Mwanahalima Adams, Lydia Akoth, Judith Musimbi, Lilian Adera, Janet Moraa, Mercy Achieng, Gererder Akinyi, Phoebe Oketch, Neddy Atieno, Teresa Engesha, Juliet Auma, Winfred Achieng, Winnie Kanyotu, Esther Nandika, Jackline Musula, Florence Awino na Lucy Mukhwana.
Maelezo zaidi na -Simon Ngaira.


Post a Comment

Previous Post Next Post