wanasoka wa Harambee Starlets Vivian Corazone (kushoto) akisherehekea na mwenzake timuni Anne Aluoch baada ya kufunga dhidi ya Misri kwenye mehci ya kirafiki ugani Safaricom Kasarani, Oktoba 28, 2016. Kenya kwenye ngoma hiyo ilishinda kwa bao 1-0. Picha/Maina Wambugu/www.sportpicha.com

Timu ya taifa ya soka kwa akina dada chini ya miaka 20 maarufu Harambee Starlets ililimwa mabao 2-1 na timu ya taifa ya wanaume chini ya miaka 13 kwenye mechi ya kirafiki iliyopigwa hapo jana uwanjani kenyatta Machakos.
Mechi hiyo ilisakatwa kwa minajili ya kuwaandaa vipusa hao kwa ziara ya nchini Jordan itakaposhiriki mechi mbili za kirafiki na wageni hao mnamo Agosti 29 na 31.
Kocha wa timu hiyo Ann Aluoch alisema kipigo hicho kilitokana na kuwakosa wachezaji wake 7 mahiri waliokuwa kwneye kikosi kilichoiwasha Botswana mabao 7-1 katika duru ya kwanza,raundi ya makundi kufuzu kwa kombe la dunia mwakani.
Saba hao wamo mjini Gulu Uganda wakiziwajibikia timu zao katika ubingwa wa Afrika Mashariki baina ya shule za upili.
Mechi hizo zinanuia kuiandaa Starlets kwa mtanange wa raundi ya pili kufuzu kwa kombe la dunia dhidi ya Ethiopia kati kati mwa mwezi ujao jijini Adiss Ababa.
Imekuwa siku yenye shughuli nyingi hapo jana, nawapongeza vijana wa Stars kwa ushindi huo,najua wametokea Uingereza waliposhinda taji la Southampton shiled.
Sasa tunataka kuwapa nafasi ya kung’ara zaidi kupitia mechi za kirafiki na timu za akademia za haiba kubwa. Alisema Adrieaus Spier, mkurugenzi wa kamati ya kiufundi katika shirikisho la soka nchini Kenya FKF. 

Post a Comment

Previous Post Next Post