Rais wa FKF, Nick Mwendwa. Picha/Stafford Ondego/www.sportpicha.com
Rais wa FKF, Nick Mwendwa. Picha/Stafford Ondego/www.sportpicha.com
Rais wa shirikisho la soka nchini Kenya FKF Nick Mwendwa ameunga mkono kauli ya shirikisho la soka barani Afrika CAF kuwa Kneya haiku tayari kuandaa kipute cha CHAN mwaka wa 2018.
Huku CAF ikitarajia kutuma waangalizi nchini kukagua maandalizi ya ubingwa huo Mwendwa alijikakamua kujibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari huku waziri wa michezo DKT.Hassan Wario akisusia kikao hicho na waandishi.
Aidha Mwendwa alieleza imani kuwa maandalizi yanaendelea vyema huku wanakandarasi wote waliotwikwa jukumu la kukarabati viwanja wakifanya kazi yao bila kusukumwa ili kuafikia makataa.
kumekuwa na tetesi kuwa Chan itapelekwa taifa jingine.Ukweli wa mambo ni kuwa lazima kuwe na wazo la pili hiyo maana CAF imetaja mataifa mengine kuwa tayari kwa uandalizi huo endapo Kenya haitakuwa tayari. Alisema Mwendwa.
Mwendwa ameongeza kuwa viwanja 11 vya kufanyia mazoezi vinahitajika kwenye kipute hicho kando na vile vitano vikuu.
Angola, Burkina Faso, Cameroon, Congo Brazzaville, Equatorial Guinea, Ivory Coast, Kenya, Libya, Mauritania, Morocco, Namibia, Nigeria, Sudan, Uganda, Guinea na Zambia ni mataifa yaliyofuzu kwa kipute hicho kilichoanzishwa mwaka wa 2008 ili kuwapa wanaoska wa ligi za mataifa yao barani nafasi ya kupiga soka la ushindnai.


Post a Comment

Previous Post Next Post