Zlatan Ibrahimovic akisherehekea bao kwenye moja wapo ya mechi za ligi kuu Uingereza msimu uliopita, akivalia pamba na Manchester United. Picha/Getty Images
Zlatan Ibrahimovic akisherehekea bao kwenye moja wapo ya mechi za ligi kuu Uingereza msimu uliopita, akivalia pamba na Manchester United. Picha/Getty Images
Mshambulizi wa zamani wa timu ya taifa ya Uswidi Zlatan Ibrahimovic amesajiliwa tena na klabu ya Manchester United kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Ibrahimovic, mwenye miaka 35 alisakatia United mechi 46 msimu jana na kucheka na wavu mara 28 wakati huo akipachika mwilini jezi nambari 9 mgonogni ila msimu huu atavalia nambari 10 aliyoizoea mshambulizi wa Everton Wayne Rooney  kwani 9 aliyokuwa ameizoea imetwaliwa na sajili mpya timuni Romelu Lukaku.
Ibrahimovic mnamo mwezi juni aliondoka rasmi Man United baada ya kumaliza mkataba wake alipoumia goti na hivyo anatarajiwa kupona na kurejea uwanjani mwezi disemba.
kufuatia mchango wake msimu uliopita anastahili kurejea. Kuvuna jeraha ni pigo ndio ila tutamvumilia hadi apone na kurejelea hali yake ya kawaida.’ Alidai meneja wa United, Jose Mourinho.

Ibrahimovic aliwindwa sana na klabu shiriki za ligi ya MLS nchini Marekani, LA Glalaxy na Los Angeles FC.
ililikuwa nia yangu na klabu kwamba nisalie 

Mwanasoka huyo mahiri alianza soka la malipo mjini kwao Malmo Uswidi na klabu ya malmo mwaka 1999 kabla ya kuisakatia Ajax, Juventus, Inter Milan, Barcelona, AC Milan na PSG.

Tangu mwaka wa 2001, Ibra amekuwa akitwaa kombe kila mwaka ikiwa ni pamoja na mataji ya ubingwa wa ligi za mataifa 13.

Hata hivyo alistaafu kwenye soka la kimataifa baada ya fainali za Euro mwaka wa 2016 ambapo amefunga jumla ya magoli 62 katika mechi 116 akivalia pamba ya timu ya taifa ya Uswidi.


MATAJI YALIYOTWALIWA NA IBRAHIMOVIC;

Ajax:
Eredivisie (2001-02, 2003-04),
Dutch Cup (2002)
Dutch Super Cup (2003)

Juventus:
Serie A (2004-05, 2005-06)

Inter: Serie A (2006-07,
2007-08, 2008-09)
Italian Super Cup (2006, 2008)

Barcelona:
La Liga (2009-10), Spanish Super Cup (2009, 2010),
Uefa Super Cup (2009), Fifa Club World Cup (2009)

AC Milan: Serie A (2010-11) Italian Super Cup (2011)

PSG: Ligue 1 (2012-13, 2013-14, 2014-15, 2015-16),
French Cup (2015, 2016), League Cup (2014, 2015, 2016) French Super Cup (2013, 2014, 2015)

Man Utd:
Community Shield (2016), League Cup (2016-17), Europa League (2016-17)


Post a Comment

Previous Post Next Post