Kyale Walker akitimuliwa uwanjani kwenye mechi dhidi ya Everton jumatatu ya Agosti 21. Picha/Getty Images
Kyale Walker akitimuliwa uwanjani kwenye mechi dhidi ya Everton jumatatu ya Agosti 21. Picha/Getty Images

Kyle Walker ameomba msamaha baada ya kurambishwa kadi nyekundu alipokuwa akiisakatia timu yake ya Man City iliyosajili sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya Everton.

Waler aliyesajiliwa kwa kima kizito cha pauni milioni 50 msimu huu kutokea Tottenham alitimuliwa kabla ya muda wa mapumziko ugani Etihad.

Kutokana na kitendo cha jana usiku, naomba msamaha kwa mashabiki wangu na wachezaji wenzangu kiujumla. Wachezaji wenzangu walifanya kazi nzuri ya kunusuru alama moja, alisema mlinzi huyo wa timu ya taifa ya Uingereza kupitia mtandao wake wa Twitter mnamo jumanne.

Walker  alipigwa kadi yake ya kwanza ya njano dakika ya 42 baada ya kumchezea ngware Leighton Baines kisha dakika mbli baadae akagongana na Dominic Calvert-Lewin na hivyo kupigwa kadi ya pili.

City ilikuwa chini baada ya Wayne Rooney kufunga goli lake la 200 pale Walker alipopigwa kadi nyekundu ila vijana wa kocha Pep Guardiola wakamudu kulazimisha sare kutokana na goli la nguvu mpya Raheem Sterling dakika nane ngoma kukamilika.

Walker sasa atakosa safari ya City ya kuelekea Bournemouth Jumamosi hii kwenye mechi ya mwisho kabla ya ligi kuchukua mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.

Walker mwenye miaka 27 atapatikana kwenye mechi yao dhidi ya Liverpool mnamo Septemba tarehe 9.


Post a Comment

Previous Post Next Post