Marehmu Mahmoud Mohammed aliyekuwa kipa wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars. Picha/Kwa hisani ya Sumba Bwire, karani wa FKF, tawi la Pwnai kusini
Marehemu Mahmoud Mohammed aliyekuwa kipa wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars. Picha/Kwa hisani ya Sumba Bwire, karani wa FKF, tawi la Pwani kusini
Aliyekuwa kipa wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars mkongwe Mahmoud Mohammed ameaga dunia.Kulingana na ripoti, atazikwa alasiri ya leo katika maziara ya Allidina karibu na hospitali kuuya pwani maarufu  Coast General.

Mwendazake aliaga dunia hapo jana usiku akiwa na miaka 68  nyumbani kwake Sega, hii ni baada ya kurejea kutoka India alipofanyiwa matibabu ya ziada. 

Mahmoud Mohammed aliyeishi Mombasa aliugua kiharusi na ugonjwa wa moyo na kulazwa kwa siku kadhaa.

Mohammed aliidakia Stars kwenye kombe la Gossage miaka ya 70 akiwa na Joe Kadenge, Jonathan Niva, William Chege Ouma na marehemu  James Sianga. 

Ametajwa kama moja wapo ya makipa bora kuwahi kushuhudiwa katika ukanda wa pwani akiwa pamoja na somo yake Mahamoud Abbas maarufu Kenya One.

Mahmoud alicheza pamoja na Anthony Makunda, Kadir Farrah, Ahmed Breik, John Nyawanga, James Siang'a , Dan Anyanzwa miongoni mwa wengine.

Abbas mwaka jana aliwasilisha wito kwa serikali kuu akiwemo rais Uhuru Kneyatta alipokuwa akisaka usaidizi wa fedha za kugharamia matibabu yake nchini India na wito huo ukapokelewa na Rais aliyetoa mchango wa pesa taslimu kisha baadae akamchangia mkongwe Joe Kadenge.

Marehemu ambaye ni baba wa watoto wanne aliisakatia Stars baina ya mwaka wa 1968 na 1974 baada ya kugunduliwa kwa talanta yake akiwa na miaka 19 alipomaliza masomo katika shule ya Arab Boys na ile ya upili ya  Khamis.

Alipiga soka lake la kwanza dhidi ya Zanzibar Tanzania kwenye dimba la Afrika Mashairki akiwa na miaka 23 kabla ya kujiunga na timu ya taifa kwenye kipute cha mataifa bingwa Afrika mwaka wa 1972 kilichoandaliwa nchini Cameroon.

Mahmoud alitembelea mataifa mengi ikiwemo Ujerumani alipokaa huko kwa kipindi cha mwezi mmoja unusu kabla ya kurejea nyumbani mwaka wa 1999. 

Alipata maumivu ya moyo mwaka wa 2005 kabla ya kuandamwa na kiharusi mwaka wa 2015 ugonjwa uliomfanya kupooza upande mmoja wa mwili.


Post a Comment

Previous Post Next Post