Afisa mkuu mtendaji wa FKF Robert Muthomi. Picha/Oliver Ananda/www.sportpicha.com
Afisa mkuu mtendaji wa FKF Robert Muthomi. Picha/Oliver Ananda/www.sportpicha.com
Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) limerefusha muda wa leseni kwa klabu zote 24 zinazoshiriki ligi kuu soka nchini (KPL) hadi Disemba 31 mwaka ujao wa 2018 ambapo timu hizo zitahitajika kukata leseni mpya na shirikisho hilo mwaka wa 2019.

Kulingana na afisa mkuu mtendaji wa shirikisho hilo Robert Muthomi, klabu hizo zitapewa muda zaidi wa  kuenenda na sheria mpya za shirikisho hilo, kisha ziwasilishe ombi la lesseni mpya  kuanzia Machi 1 hadi Juni 30 mwaka ujao wa elfu 2018. 
Tungependa kujulisha timu zote zinazoshiriki ligi kuu ya humu nchini kuwa jopo letu limeongeza muda wa makataa wa kukata leseni mpya kwa timu zinazoshiriki taji la FKF hadi Disemba 31/2018, kwenye msimu mpya wa mwaka wa 2019. Alisema Muthomo.
Kwenye leseni za msimu huo wa 2019, timu zote  zitapewa makataa ili kufanya uamuzi wao kwa sheria na vigezo vipya kuhusu leseni hizo kutoka kwa jopo la FKF msimu huo na hiyo ni  kuanzia Machi 1 hadi Juni 30,2018, tarehe itakayolandana na mechi za CAF.
Makataa ya mwisho yatakuwa Octoba 31, 2018, Alimalizia afisa huyo mkuu.


Taarifa zaidi kutoka kwake Simon Ngaira
Post a Comment

Previous Post Next Post