Uga wa Kasarani, Nairobi. Picha kwa hisani ya Enos Teche
Uga wa Kasarani, Nairobi. Picha kwa hisani ya Enos Teche
Kampuni ya KPL, inayosimamia na kuendesha ligi kuu soka taifa Kenya kwa mara nyingine italazimika kuratibu mechi zake nje ya jiji la Nairobi muda huu hadi mwaka wa 2019.

Nyuga za Nyayo na Kasarani baada ya mechi za leo hazitapatikana kwani zitafungwa ili kuruhusu shughuli ya ukarabati wa kujipanga kwa kipute cha mwaka ujao cha CHAN kitakachoandaliwa humu nchini.

Uwanja wa Nyayo ushaanza kukarabatiwa ila utaandaa mechi yake ya mwisho hapo kesho baina ya AFC Leopards na Tusker FC.

Uwanja wa Kasarani utaandaa mechi yake ya mwisho hii leo baina ya Posta Rangers na Gor Mahia.

Hii ni mara ya pili nyuga hizo za haiba kubwa kutopatikana na hivyo italazimu mechi hizo zihamishiwe katika nyuga za Thika, Nakuru, Narok, Machakos na Kisumu.

Post a Comment

Previous Post Next Post