Wakenya Linet Masai (kushoto) na Emily Chebet (kati) npamoja na Methiopia Meselech Melkamu (kulia) wakituzwa medali zao baada ya kumaliza katika nafasi za 1-3 ubingwa wa  Iaaf World Cross Country jijini ydgoszcz, Poland Machi 28, 2010. Picha/Michael Steele/Getty Images Uropa
Wakenya Linet Masai (kushoto) na Emily Chebet (kati) pamoja na Methiopia Meselech Melkamu (kulia) wakituzwa medali zao baada ya kumaliza katika nafasi za 1-3 ubingwa wa  Iaaf World Cross Country jijini ydgoszcz, Poland Machi 28, 2010. Picha/Michael Steele/Getty Images Uropa
Linet Masai atapokea medali ya shaba ya mashindano ya olimpiki mwaka wa 2008, ikiwa ni miaka tisa baada ya muda wake wa dakika 30:26.50 kutosha mboga kumpatia ubingwa wa dunia kwa chipukizi na pia wa taifa..

Masai ambaye ni bingwa wa mwaka wa 2009 kwenye masafa ya mita 10,000 na aliyemaliza wa nne jijini Beijing, alizawadiwa nishani hiyo kufuatia kufungiwa kwa mshindi wa pili mturuki Elvan Abeylegesse aliyenaswa na hatia za utitimuaji misuli.

Abeylegesse alipatikana na hatia hiyo ya kutumia pufya kwenye uchunguzi wa sampuli za chembechembe za damu na mkojo kwa mwanariadha huyo mzawa wa Ethiopia kutoka kwa ubingwa wa ulimwengu mwaka wa 2007 huku tangazo hilo likiwasilishwa miezi mitano.


Mwanariadha wa masafa marefu wa Uingereza Shalane Flanagan hapo jana alikuwa wakisherehekea baada ya kuzawadiwa nishani ya fedha ila akadai hataki kufanyiwa sherehe ya kukabidhiwa medali hiyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post