Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger. Picha/Getty Images
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger. Picha/Getty Images

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuzidi kuwa na imani na timu na kuendelea kuishabiki licha ya kubamizwa kichapo kizito cha mabao 4-0 mikononi mwa Liverpool kwenye kipute cha ligi kuu soka taifa Kenya KPL hapo jana jioni ugani Anfield.

The Gunners wanavyofahamika katika jina lao la kupanga hawakufyatua hata shuti moja lililolenga goli na badala yake walitandaza soka mbovu iliyowaudhi mashabiki wengi waliokuwa wakiifuatilia ngoma hiyo.
Iwapo kuna wale wanaodhani mimi ndio mzigo kwneye timu hii, basi wanataka radhi,”Wenger aliambia tovuti ya Sky Sports.
Tunataka mashabiki wetu wadumishe upendo nasi hata baada ya uchezaji mbaya hivyo na kushindwa."
Jambo pekee ambalo tunaweza kufanya ni kurejea na kucheza vyema.
Wenger  alitia saini mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa msimu uliopita, licha ya baadhi ya mashabiki kumshutumu aondoke.
Timu hiyo aidha ilimaliza ligi msimu uliopita katika nafasi ya tano na kufungiwa nje ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 21 ambayo wamekuwa na Wenger licha ya kufaulu kushinda Kombe la FA.
Alexandre Lacazette kinda aliyetwaliwa timuni humo kwa kitita kikuu aliachwa na kocha huyo kwenye benchi kwenye mechi hiyo ya jana na akamwanzisha Alexis Sanchez aliyeanza mechi yake ya kwanza tangu kufunguliwa kwa msimu.
Liverpool walisajili alama tatu muhimu kupitia magoli yao Roberto Firmino, Sadio Mane, Mohamed Salah na Daniel Sturridge.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger. Picha/Getty Images
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger. Picha/Getty Images

Hatukuwa katika kiwango kifaacho tangu dakika ya kwanza kimwili, kiufundi na kiakili  na tuliadhibiwa," alisema wenger ambaye ni raia ya Ufaransa baada ya mpambano huo.
Uchezaji wetu leo haukubaliki. Ni kweli kwamba leo tulikuwa wapinzani wepesi kwa Liverpool.
Uchezaji wetu ulikuwa mbaya mno sana.Sitaki kutekwa na hisia, lakini tuna safari ndefu, na kuna sababu zinazosababisha hilo, na wachezaji sasa wanaelekea kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa, lakini lazima tujifunze kutokana na uchezaji wetu leo."


Post a Comment

Previous Post Next Post