Foyd Mayweather (Kushoto) na Conor McGregor (Kulia) Picha/Kwa hisani
Conor McGregor  ametabiri kuwa atamtambariza Floyd Mayweather  kwenye raundi ya kwanza tu, McGregor mwenye miaka 29 akizungumza na tovuti ya Sky Sports, alisisitiza kuwa atamuaribu Floyd Mayweather kwenye raundi ya kwanza ya pigano la uzani mzito litakalo andaliwa Agosti 26 katika ukumbi wa T-Mobile Arena jijini Las Vegas, Marekani.

McGregor aliyekuwa akizungumza kwa hamasa, amesema kuwa yu tayari maana anayafahamu makeke ya Mayweather, na kwa maana hiyo hatampa nafasi ya kupumua akiwa kwenye kamba.

Kwa sasa naeza sema niko sawa na kawaida yangu huwa tayari  kwa kila pigano. Nitamchakachua Mayweather katika dakika za mwanzo mwanzo tu la pigano maana hiyo ndio biashara yangu kubwa,” alisema McGregor. 

Najua naye si mchache, kwa kuwa kawaida yake yeye huwa makini kwa raundi ya kwanza, ila niseme kuwa hii itakuwa siku nyingine kwangu kudhirishia ulimwengu ninachoweza kukifanyaItakuwa ni siku nyingine, pigano jingine na wakati mwingine ambao nimeishi kusubiria, nilishamtandaza mara moja na hii itakuwa mara yangu ya pili, na nina uhakika atajutia akiwa ulingoni,” aliongeza mwanandondi huyo maarufu.
McGregor  anayeshiriki pigano la uzani mzito alisema kuwa alifurahia kipindi kile akimgaragaza Meyweather huku akishangiliwa na mashabiki wa Ireland waishio Las Vegas na kwamba hili litajitokeza raundi hii, hali itakayompa msukumo  wa kunyanyuka na ushindi mapema.
Mayweather kwa upande wake alihoji kuwa yu tayari na hatishiki na kidomo domo cha McGregor na kwamba atamuondoa mapema kwenye mchezo ili kujihakikishia ushindi wake.
Aliongeza kuwa ushindi wake ni furaha kubwa kwa mashabiki wake na kwa maana hiyo atafanya kila awezalo kuwapa ushindi huo baada ya kutinga kwenye awamu ya fainali kwa kumuondoa Manny Pacquiao jumamosi iliyopita.
Niliwaelezea kabla ya pigano langu na Pacquiao kuwa haitanichukua muda mwingi kumuondoa kwenye mchezo, kitu ambacho nilitimiza kwa ajili ya mashabiki wangu.

Najua mashabiki wanataka kuona jasho, machozi na damu na hicho ndicho watakachokiona usiku wa jumamosi hii,” aliongezea Meyweather.
Aidha alimsuta McGregor kwa kumtaja kama kuku muoga.
Najua kuwa hulka yake ni kuoneshana meno yake kwa hasira zake kama za kuku, ila hilo halinitishi mimi nitawapa mashabiki wangu wanachokitarajia. Meyweather alimalizia.
Maelezo zaidi kutoka kwa Simon Ngaira 
Post a Comment

Previous Post Next Post