Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga  akimla chenga Tisserand Marcel wa Congo wakati wa mechi ya kimataifa ya kirafiki uwanjani Keyatta Machakos mnamo Machi 26, 2017. Harambee Stars ilishinda kwa mabao  2-1. Picha/Jeff Angote
Mshambulizi wa Harambee Stars Michael Olunga  akimla chenga Tisserand Marcel wa Congo wakati wa mechi ya kimataifa ya kirafiki uwanjani Keyatta Machakos mnamo Machi 26, 2017. Harambee Stars ilishinda kwa mabao  2-1. Picha/Jeff Angote

Mshambulizi wa timu ya taifa ya soka Harambee Stars Michael Ogada Olunga ametua kwenye klabu ya Girona FC ya Uhispania kwa mkopo akitokea Guizhou Zhicheng ya Uchina.
Mwanasoka huyo mwenye miaka 23 amekuwa akisisitiza kuhamia Uhispania baada ya kuozea benchi akiwa klabuni Guizhou.

Uhamisho wa kijulanga huyo unajiri baada ya aliyekuwa kocha wake wa zamani kule Uchina Gregorio Manzano kumsulubisha timuni ili kuwanasa washambulizi Ruben Castro Mario Suarez kutokea Uhispania.

Kugura kwa mhandisi huyo zamani akiwasakatia viongozi wa ligi kuu soka taifa Kenya KPL hadi sasa Gor Mahia na Djurgardens ya Uswidi kumetarajiwa na mashabiki wengi wa soka nchini ambao hawakufurahishwa na hatua ya kukalishwa benchi Uchina.


Olunga alitakiwa kurefushiwa mkataba wake na timu ya awali hatua iliyofeli na kumghadhabisha sana Olunga.


Isitoshe, inaaminika hiyo haikuwa inamruhusu Olunga kucheza na wenzake na kumlazimu afanye mazoezi na kikosi chipukizi hadi Disemba tarehe 31 kutokana na sheria za shirikisho la soka Uchina, hali ambayo haikuwa inampa utulivu klabuni hapo.  


Olunga aliwahi kueleza hisia zake za kurejea kwake barani Uropa akiwa na miamba wa Ufaranza Olympic Lyon, hii ikiwa na maana kuwa alikuwa tayari kugura klabuni humo.


Ujumbe sawa na huo ulihoji kuwa kwamba mshambulizi huyo Skwa sasa atahamia kwenye moja wapo ya klabu za Katalunya, hii ni kutokana na yeye kuonekana kwenye moja wapo wa uwanja kule akishuhudia mpambao wa timu yake hiyo mpya na Malaga ugani Blash Hossein.


Ikiwa mkataba huu utaafikiwa na pande husika, huenda ukawa wa kipindi kirefu, ilihoji tuvuti ya Uhispania ijulikanayo kama Marca.com.Hata hivyo Olunga tayari ashaonyesha ari yake ya kuwa na timu hiyo iliyoanzishwa mwaka 1930, iliyoko eneo la Girona, kule Katalunya.

Hata hivyo timu hii ilipanda ngazi hadi kwenye ligi ya La Liga katika msimu wa mwaka wa 2016/2017.


Uwanja wa nyumbani wa timu hiyo unaitwa Estadi Montilivi, unaobeba mashabiki wapatao 13,500 waliokaa na kutulia.
 Uandishi zaidi kutoka kwa – Simon Ngaira.

Post a Comment

Previous Post Next Post