Wadau wa KPL, kampuni inayosimamia na kuendesha  ligi kuu nchini wakiizawidi Tusker FC kombe msimu wa 2016. Picha/Kwa hisani
Wadau wa KPL, kampuni inayosimamia na kuendesha  ligi kuu nchini wakiizawidi Tusker FC kombe msimu wa 2016. Picha/Kwa hisani
Jumla ya mechi sita za kuwinda ligi kuu soka taifa Kenya KPL zimeratibiwa kugaragazwa hii leo katika nyuga mbali mbali.

Sofapaka watagaragazana na Nzoia Sugar FC katika uga wa Kasarani kuanzia saa nane alasiri, Kakamega Homeboys wacheze na Bandari ugani Mumias saa tisa.

Kariobangi Sharks kwa upande wao watapigane na Western Stima huko Kenyatta Machakos majira yayo hayo, kisha Mathare wacheze na Nakumatt uwanjani Ruaraka.

Sony Sugar watapepetana na Zoo FC huko Awendo alafu Gor Mahia wapambane na Posta Rangers uwanjani Kasarani,mechi ambayo itaanza saa kumi na robo alasiri.


Mechi moja pekee imerangwa hapo kesho na itakutanisha AFC Leopards na Tusker katika uchanjaa wa Kasarani.

Post a Comment

Previous Post Next Post