Mshindi wa medali ya dhahabu Nick Okoth akiwa mazoezini,Picha kwa hisnai ya Standard Digital
Mshindi wa medali ya dhahabu Nick Okoth akiwa mazoezini,Picha kwa hisnai ya Standard Digital

Timu ya taifa ya ndondi iliyoko Ujerumani kwa sasa kushiriki mashindano ya dunia ya AIBA mwaka huu inasubiria tu droo ili kuanza mizuka ya kusaka medali kwa taifa kuanzia Agosti 25 hadi Septemba 3.

Kulingana na Kameta, wanandondi watatu wanaotarajiwa kuipeperusha bendera ya Kenya katika mashindano hayo, wapo nchini ujerumani kwa sasa wakifanya mandalizi ya mwisho mwisho.
Kwa sasa tunasubiria AIBA kutoa droo ya mapigano hayo muda wowote kuanzia sasa, ili tuweze kubaini wapinzani wetu,” alihojo Kameta.Wanandondi wetu walio jijini Hamburg, wanajifua dakika za lala salama na kujizoesha na hali ya anga. Hawajaenda kule kujivinjari.Aliongeza mwenyekiti huyo.
Kameta amepongeza juhudi za shirikisho la ndondi nchini kwa kusema liliandaa mchujo mzuri katika kukiunda kikosi anachoamini kitafana kwenye mapigano ya kimataifa na kuwa walikitengea muda wa kutosha wa kunjiandaa sawa na kuwalipa marupurupu yao.

Aidha aliongeza kuwa kufikia sasa hawana panda shuka zozote, isipokuwa hofu ya mabadiliko ya hali ya anga ambapo kwa wakati mwingi hutatiza na kuyumbisha timu nyingi.
Kuwasili mapema Ujerumani kumeipa timu nafasi nzuri ya kujizoesha na hali ya anga iliyo tofauti na ya Nairobi. La msingi hapa ni kuzingatia ulichokifuata huko, Kwa mfano unaweza kuwekwa pamoja na bingwa mtetezi kwenye mchezo, la muhimu ni kuzingatia mafunzo kutoka kwa mkufunzi na wala si kujipanga ukiwa kwenye ukumbi wa Sporthalle Arena. Alisaili fundi huyo.
Kikosi ambacho kitapeperusha bendera ya Kenya kitawakilishwa na mshindi wa nishani ya dhahabu Nick Okoth ambaye alimsasambua Reda Benbaziz kutoka Algeria kwenye uzani wa lightweight.

Maelezo ya ziada kutoka kwa -Simon Ngaira

Post a Comment

Previous Post Next Post