Azarenka akishiriki ubingwa wa U.S Open awali.Picha kwa hisani
Azarenka akishiriki ubingwa wa U.S Open awali.Picha kwa hisani

Nyota wa tenesi kwa upande wa wanawake Victoria Azarenka atalazimika kukaa nje ya mashindano makuu ya wazi nchini Marekani.
Azarenka mwenye ukuu wa miaka 28 hatoshiriki mashindano hayo yatayofungua pazia zake Agosti 28, hii ni kutokana na sababu za kifamilia kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari.
"Nasikitika sitaweza kushiriki mashindano ya wazi ya Marekani mwaka huu kutokana na hali yangu ya kifamilia inayoendelea kwa sasa," Azarenka alinukuliwa akisema  Jumatatu ya Agosti 21.
Mwanatensi huyo matata alirejea katika ulingo wa mchezo huo mwezi wa sita mwaka huu baada ya kuwa mkekani kwa muda baada ya kuwa mjamzito mwezi Disemba na kujifungua salama hii leo.Post a Comment

Previous Post Next Post