Wing'a wa Borrusia Dortmund Ousmane Dembele. Picha/Getty Images
Wing'a wa Borrusia Dortmund Ousmane Dembele. Picha/Getty Images
Huenda mchezaji wa Borussia Dortmund ya Ujerumani Ousmane Dembele akawa mwanasoka wa pili ghali endapo mpango wa kutokomea klabuni Barcelona utafaulu.
Barca iliwaislisha ombi kwa Borussia Dortmund kuhusu mchezaji huyo mwenye miaka 20 ambalo baadae lilikataliwa kwani thamani yake inakisiwa kuwa Euro milioni 100 mapema mwezi Agosti mwasoka huyo alipopigwa marufuku kwa kudinda kufika mazoeizni.
Kitita hicho aidha kinakadiriwa kuwa chini ya  Euro milioni 222 zilizotumiwa na PSG ilipomsajili Neymar kutoka Barcelona mwezi Agosti.
Kiwango cha fedha hizo kitazidi kile kilichowasilishwa na Manchester United kumtwaa Paul Pogba kutoka Juventus. Dembele anayechezea timu ya taifa ya Ufaransa hajaonja mechi akiwa na Dortmund tangu ashiriki kombe la Super cup mnamo Agosti 5.
Ujio wake klabuni Dortmund ulitokea Rennes kwa kitita cha Euro milioni 15 yapata mwaka mmoja uliopita.


Post a Comment

Previous Post Next Post