Mwanariadha David Torrence.Picha/ Getty Images
Mwanariadha David Torrence.Picha/ Getty Images

Mwanariadha wa mbio za masafa ya wastani kutoka Marekani David Torrence amepatikana amefariki katika kidimbwi cha kuogelea jimboni Arizona.

Torrence aliyefariki akiwa na miaka 31, alishinda fedha katika mbio za ubingwa wa dunia za kupokezana vijiti mwaka 2014 na alimaliza wa pili pia katika mbio za bara la Amerika mwaka 2015.


Hata hivyo, alibadilisha uraia kutoka Marekani hadi Peru na akawakilisha taifa hilo lake jipya katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016.

Wachunguzi wa jinai wamebaini kwamba hakuna dalili zozote dhahiri kwamba huenda aliuawa," taarifa ya polisi imesema.

David Torrence alimaliza wa 13 mbio za 5,000m upande wa wanaume katika michezo ya Olimpiki ya Rio mwaka 2016 ambapo Mo Farah alishinda dhahabu.

Maelezo zaidi kutoka kwa BBC Swahili

Post a Comment

Previous Post Next Post