Chipukizi wakipiga zoezi la mpira wa vikapu.Picha kwa hisani ya 'The Giants of Africa'
Chipukizi wakipiga zoezi la mpira wa vikapu.Picha kwa hisani ya 'The Giants of Africa'

Washirikishi wa mchezo wa vikapu wanaendelea na mpango wao wa kuzunguka mataifa ya bara Afrika  huku wakiwamotisha vijana wenye talanta Afrika.
Washirikishi hao kutoka kwa mpango makhusisi wa maendeleo barani yaani  ‘The African Giants development program’ ukipenda "The Giants of Africa” walikuwa nchini kuanzia Agosti 13 hadi 15 mwaka huu kabla ya kuelekea nchini Nigeria kwenye kampeni yao ya kukuza na kuendeleza vipaji Afrika.
Kwa sasa wanaendelea na mikakati ya kuzuru mataifa mengine Afrika lengo kuu likiwa kuuendeleza mchezo wa vikapu, kama ngao ya kuwakuza vijana wa kiafrika, sawa na kuwahamasisha kushikilia na kuendeleza ndoto na malengo yao maishani.
Insongo Iboh, mkurugenzi mkuu wa mpira wa vikapu katika kanda hii ya Afrika mashariki, amedokeza kuwa, walikuwa na wakati mzuri hapa Kenya, ambapo waligundua vipaji vingi kati ya miaka 14 hadi 18 na kwamba shirika hilo limejitolea kuwasaidia vijana waliotambuliwa kukuza talanta zao.

Kipindi tukiwa Kenya,lengo letu kuu lilikuwa kuwasaidia vijana wetu wa kiafrika. Tuliwapa mafunzo kabambe wale tuliogundua vipaji vyao na tunaamini usaidizi na mafunzo tuliyowapa yatawafaa sana kwenye maisha yao ya baadaye. Alisema Iboh.

Kulingana na Iboh, “The Giants of Africa” imejitolea pakubwa kuhakikisha inakuza na kuendeleza mchezo wa vikapu Afrika ili kuwawezesha kukusanya talanta kutoka mataifa yote ya Afrika.

Aidha shirika hilo linajihusisha na mpango wa kutengeza na kuendeleza kambi za mpira wa vikapu humu nchini na kimataifa.

Iboh aliongeza kuwa walipokuwa humu nchini, shirikisho pia liliwapa wakufunzi mafunzo, lengo kuu likiwa kuwaongezea ujuzi sawa na kuwawezesha waelewe mchezo na wachezaji wa kiafrika sawa na panda shuka zinazowakabili.

Iboh amedokeza kuwa “The Giants of Africa” pia huwaleta pamoja wakufunzi na makocha wanaoinukia kutoka pembe zote za dunia kwenye kambi za shirika hilo kote ulimwenguni, ili kubatilishana mawazo kuhusu mchezo wa vikapu ulimwenguni.

 Kulingana na Iboh, tangu “Giants of Africa kuundwa imehudumu kwa zaidi ya miaka 14 nchini Nigeria, sawa na kuhudumu miaka 4 hapa nchini Kenya.

Lina zaidi ya wachezaji 100 wa mpira wa vikapu ambao baadhi yao ni wanafunzi wa vyuo vikuu kule Marekani na wengine wao wakiwa wachezaji tajika kwenye vilabu kadhaa vya mchezo huo barani Uropa.

Shirika hilo kupitia udhamini mbali mbali limefanikiwa kutembelea kambi zao zilizoko Rwanda mnamo Agosti 7 hadi 9, Uganda kuanzia Agosti 10 hadi 12, hapa Kenya kuanzia 13 hadi 15 Nigeria 18 hadi 20 na wanatarajiwa kuzuru hapo kesho 23 hadi 25 watazuru nchi ya Ivory Cost kisha wakamilishe gange hiyo tarehe 26 hadi 28 mwaka huu kule Senegali.


Maelezo zaidi kutoka kwa – Simon Ngaira

Post a Comment

Previous Post Next Post