Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Thiery Henry. Picha/Getty Images
Mshambulizi wa zamani wa Arsenal Thiery Henry. Picha/Getty Images
Aliyekuwa mshambulizi matata wa klabu ya Arsenal Thierry Henry, amewasuta wanasoka wa Arsenal kwa kutokuwa makini kwenye mchezo baada ya kudhalalishwa na mabingwa wa Macy-side, Liverpool Fc hapo jana jioni ugani Anfield, huku akitaka kutokushirikishwa kwa vyovyote na timu hiyo ya kaskazini mwa London.

Henry ambaye alishuhudia kibano cha Liverpool kutoka kwa Roberto Firmino pamoja na Sadio Mane wakiibinikiza Arsenal mabao ya mapema kwenye kipindi cha kwanza na baadaye Mohamed Salah na Daniel Sturridge wakiwanyima mashabiki wa Arsenal raha kwenye kipindi cha pili na kufanya mambo kuwa 4-0, amehoji kuchoka na hujuma za Arsenal.   

Henry ambaye alikuwa uwanjani kushuhudia mpambano huu, anasema kuwa alitamani kuondoka uwanjani, ila miguu yake ikawa mizito kana kwamba aliikuwa imetiwa gundi.
Nilijua kutoka mapema kuwa kile ambacho kingetokea, ila sikujua itakuwa kwa kiwango hiki, kwa hivyo si eti nimeshtuka sana. 
Kinachinitia uchungu zaidi ni vile Arsenali wamekubali kibano cha magoli manne kwa nunge, hili linaonesha uzembe wa kikosi hiki na ndiyo maana sitaki tena kujishirikisha na hii timu hii.” Alisema Henry.
Mshambulizi huyo wa zamani aliongeza kuwa imekuwa vigumu kwake kushuhudia mpambano wowote wa Arsenal kwa siku za hivi karibuni. Anasema kuwa alipokuwa hapo kikosini alijitolea kwa hali na mali kufa na tumu hiyo, kitu ambacho hakifanyiki siku za sasa. 

Alizungumzia kujikokota kwa wachezaji kama Alexis Sanchez ambao bado wanashikiliwa na kocha Venga, kitu ambacho kinairudisha nyuma timu hiyo kuu ya Uingereza.
Ni uchungu kwetu sisi kama washirika dau na mashabiki shakiki wa Arsenal. Inakuwaje vitu ambavyo vinafanyika pale Arsenal ni vitu ambavyo vimekuwa vya kujirudia kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.
Kwa mfano nikizungumzia Sanchez ambaye anashawishiwa kubakia pale Arsenal ilihali ana hamu ya kugura, swali ni jee, ataweza kuwa na muda mzuri pale kikosini?
Hii ndiyo maana wachezaji wengi pale hawataki kuongezea mkataba wao, kumaanisha kuwa kuna kitu ambacho si kizuri kinachoendelea kwenye kambi ya Arsenal.” Alimalizia mchezaji huyo matata wa Arsenal.

Ripoti ya ziada kutoka kwa Simon Ngaira

Post a Comment

Previous Post Next Post