Kocha wa AFC Leopards Robert Matano akitoa ishara kwa wachezaji wake kwenye moja wapo ya mechi za ligi kuu KPL. Picha/Kwa hisani
Kocha wa AFC Leopards Robert Matano akitoa ishara kwa wachezaji wake kwenye moja wapo ya mechi za ligi kuu KPL. Picha/Kwa hisani
Mkufunzi wa AFC Leopards Robert Matano amesema vijana wake wako tayari kwa mpambano wa Jumapili dhidi ya mahasimu wao wa jadi Gor Mahia, baada ya kulemea mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini Tusker FC goli moja kwa bila jana jioni.

Samuel Ndung’u alipachika wavuni goli hilo la pekee dakiak ya 82, na kuipa Ingwe ushindi sawa na wa Gor Mahia hapo juzi dhidi ya Posta Rangers, zikisalia siku mbili pekee timu hizo zikutane uwanjani wa kitaifa wa Nyayo.

Matano aidha amesisitiza nidhamu ni kigezo kikuu katika harakati za kurejeshea Leopards hadhi yake ya zamani.
Timu iko katika hali shwari na unaweza kuona matokeo si mabaya sana. 
Mashemeji derby ni mchuano wa kawaida kama mechi zingine ila tutajikaza kuona tunapigania hadhi ya klabu yetu kwa kuwafunga Gor Mahia.
Wachezaji lazima wajitume kwa hiyo mechi,ninahitaji heshima na nidhamu ya hali ya juu nje na ndnai ya uwanja.
Lazima wachezaji wangu wafanye mazoezi kila siku,kuna baadhi ya wale waliokuwa wakija mazoezini watakavyo, tangu kuchukua hatamu za kuiongoza Ingwee nimeweka mikakati madhubuti ya kinidhamu kuhakikisha yeyote anayekosa mazoezi bila sababu maalum anaadhibiwa vikali. 
Mchezaji hafai kukosa mazoezi kwani sote timuni tuko sawa na tunalipwa mshahara, Alisema Robert Matano.

Post a Comment

Previous Post Next Post