Huku kipute cha CHAN kitakachoshirikisha wachezaji wa ndani wa ligi za mataifa mbali mbali barani Afrika kikikaribia mwaka ujao wa 2018, maswali mengi yanaulizwa kama Kenya iko tayari kukiandaa.


Ukaguzi wa mwisho unatarajiwa mapema mwezi Septemba ilhali kuna kazi kubwa ya ukaratabi wa viwanja iliofanywa hadi sasa tangu ukaguzi wa mwisho kuandaliwa mwezi juni.


Hadi sasa ukaguzi ungali ukiendelea katika uga wa Kipchoge Keino mjini Eldoret,moja wapo ya viwanja vitakavyotumika kuandaa kipute hicho huku ukarabati ukiwa haujaanza katika viwanja vingine vinne vya Kasarani, Nyayo,Machakos na Kinoru.

Kamati andalizi ya humu nchini aidha inadai wanakandarasi wanafaa kuanza shughuli ya ukarabati huo wiki hii.

Hii leo kampuni ya Sports Kenya inafaa kukutana na wanakandarasi wote na kujadili kuhusu wepesi wa ukarabati wa nyuga hizo ili maafisa wa shirikisho la soka barani Afrika CAF watakapozuru nchini kwa ukaguzi wapate kazi inaendelea” asema mwenyekiti wa shirikisho la soka nchini FKF, Nick Mwendwa.

Wakaguzi kutoka CAF wanatarajiwa nchini Septemba 7, kwa uangalizi wa mwisho wa viwanja husika na masuala mengine na endapo hawataridhishwa na watakachokiona basi huenda Kenya ikanyang’anywa fursa hiyo huku ikikisiwa kuwa mataifa mawili ya Morocco na Afrika Kusini yako chonjo ambapo moja wapo anaweza kabidhiwa.

Kiukweli ni kuwa hatutakuwa tumetekeleza kazi ya ziada ila endapo wakaguzi watafika na kusema labda uga wa Kipchoge Keino wafaa kufanyiwa mawili matatu na wanakandarasi wanaendelea na kazi yao, sidhani kutakuwa na tatizo lolote kwani tutakuwa tumeonyesha uwezo wetu na ndicho wanachotaka kuona. Aliongezea Mwendwa. 
Rais wa FKF Nick Mwendwa kwenye ukaguzi wa uga wa Kinoru,Meru.Picha kwa hisani ya CITIZEN DIGITAL
Rais wa FKF Nick Mwendwa kwenye ukaguzi wa uga wa Kinoru,Meru.Picha kwa hisani ya CITIZEN DIGITAL
Endapo mpango wa awali utafeli, Kamati andalizi ya humu nchini na ile ya CECAFA zitaandikia CAF kuhakikisha CHAN inaandaliwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Kuna mataifa yanayoweza kutuazima uwanja wao ili tuutumie kwa baadhi ya mechi za kipute hicho, hilo ni wazo nzuri pia tunaloweza kulitumia” alisisitiza Mwendwa ambaye awali alikuwa mwenyekiti wa ligi iliyosambaratishwa ya FKF.

Jumla ya timu 15 zishafuzu kwa dimba hilo yakijumuisha wenyeji Kenya, Cameroon, Congo na Equatorial Guinea yatakazowakilisha zoni ya kati.

Sudan na Uganda zitawakilisha ukanda wa mashariki ya kati, Libya na Morocco watakuwa wawakilishi wa ukanda wa Kaskazini , Angola Zambia na Namibia watawakilisha zoni ya kusini huku Mauritania, Guinea na Senegal zikiwakilisha zoni A Magharibi alafu zoni B magharibi ikiwakilishwa na Burkina faso, Cote d’ Ivore na Nigeria. 

Hayo ndo mataifa yaliyofuzu kwa kipute hicho hadi sasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post