Diamond Platnumz| Photo By| Diamond FB

Diamond katika Zilizopenda 

Kama mdau katika maswala haya ya burudani, nimekuwa nikifatilia kwa sana hatau zote msanii Diamond Platnumz amekua akipitia. Wengi mnavyo fahamu ama kumfahamu Diamond amekua mwepesi sana kutumia fursa anayopewa na wapinzani wake pale anapogundua udhaifu wao, hutumia udhaifu huo kama ngazi na kukwea hatua baada ya hatua hadi juu anapotaka yeye. Mifano kidogo tu, alitumia mahusiano yake kutengeneza skendo ambazo kwakweli zilimunufaisha na kumkuza si kisanaa tu pekee bali kwa kutengeneza umaarufu ambao ndio chimbuko wa ufanisi katika maisha yake.


Mbali na mahusiano yake, alifanya bidii kuhakikisha kuwa hakuna msanii yeyote waliyekuwa level moja naye kwa kipindi kile anamshinda sikimawazo tu, bali kwa ubora wa kutoa mziki. Ndiposa kila uchao alihakikisha ankuja na mikakati mipya na mbinu tofauti ilikuhakikisha ndoto yake inatimia. Kila alipopata hela kwa show zake, alihakikisha kuwa hela ile haitumiki kwa starehe, ila ilitumika katika kuekeza kwenye mbinu ambazo zingemuinua nakuwa Diamond yule ambaye tunamouna leo. Hivyo kuanzia ubora wa Saauti (audio) hata video ikabidi aanze kuwekeza huko. Kitu ambacho kilimpelekea kutafuta maarifa ya madirector kutoka hapa kenya wakiwemo Ogopa videos waliomtenenezea vidoe ya ''My Number One''.Number One ilimufungulia milango mikubwa, haswa nibaada ya video hiyo kutumika kumshawishi msanii Davido wa nchini Nigeria, pale alipozuru Tanzania kwa ziara yake ya kimuziki. Kupitia AY, Diamond alishakiri kuwa alimuezesha kutimiza ndoto yake yakuenda kimataifa. Nahapo ndipo Number One remix ikazaliwa, na kwakweli Mungu hamuachi mja wake ngoma ile ikawa chanzo cha mafanikio ya Diamond kwenda kimataifa hadi zaidi. Kwahivyo wasanii wenzake waliokuwa wakishindana naye wakawachwa nyuma midomo wazi. Huku Rich Mavoko na wengine wenye kujaribu kushindana naye wakawa bado wanapambana.

Rich Mavoko| Photo By| Mavoko fb

Rich MavokoMavoko alihamia Kenya kwa lebo ya Kaka Empire, ambako alitia kidole mkataba pale na kazi ikiwa ishaanza. Pacha wangu ikazaliwa na baadaye akashirikishwa na rapper mkali kwasasa Darassa na ngoma hii pia ikawa imeanza kumuka Rich Mavoko kwenye ligi nyingine tofauti. Siwezi fahamu kulifanyika nini chini ya pazia, ila kwa mbio za farasi hizi, hazikumpa Dangote usingizi. Hivyo akiwa mwenye akili na mjanja mikakati ya kumusainisha mkataba wa miaka kumi nguli huyu wa pacha wangu lazima uliundwa, ila kwa njia ambayo Mavoko asingeshutuka. Ilimradi ionekane yeye ndie kaja pale WCB kuomba nafasi ile. Na kweli mwisho wa siku mpaka leo ''Zilizo Pendwa'' imetoka Rich Mavoko yupo mle ndani.


Diamond anafahamu fika kuwa kazi yake ya kuitawala himaya ya Bongo Flava kama Simba bado haijafaulu asilimia mia. Maana kuna nguli mmoja amenyog'onyea kipaji cha muziki, sauti na nitishio kwa upande wa kuwanasa akinadada warembo. Kitu ambacho hakija muacha salama star huyu wa Bongo Flava na si mwingine ila ni Alikaba. Uwezo wake wakuitawala media, ushawishi wake na ujanja wake pia umefunya licha ya kuwasainisha vijana wenzake WCB, pia anafanya kila awezavyo kuwavuta mastaa wakongwe kufanya kazi nao kwa ukaribu ili kupata back up. Tuwataje wachache tu, Dully Sykes, AY, Khadija Kopa, Fid Q na hata Mr. Nice kitu ambacho Alikiba kwa upande mwingine hajawahi kufikiria. Hii si bure ila kwa mtu mwenye umakinifu kwasana utagundua kuwa ni mbinu ya kujitengenezea jina na sifa didhi ya upinzami.


Alikiba| Photo By|Alikiba

Lakini hata baada ya kufanya hivyo, Diamond lengo lake la kumpiku Alikiba halijawahi kufanikiwa.Kwani cha kumuumiza zaidi, anafahamu fika kuwa Kiba anabahati ya mtende. Yeye si murahisi wa kutuoa vibao, ila kila anapotoa kibao kinadumu kwa mda mrefu, kisha hajaachwa kutajwa kwenye list za tunzo za kimataifa kila mwaka mathlani yeye. Kiba pia amekua mgumu sana wa kuongea ama kujibu mapigo ambayo Diamond, huwa anatumia nguvu kadri ya uwezo wake ilikumchokoza ndiposa amusome madhaifu yake ndio apate njia ya kumfanya ngazi na kuvaa kilemba cha ufalme wa Bongo Flava kama ilivyo kiu yake. Lakini hata hivyo Alikiba amekumjanja zaidi yake na majibu yake huwa ya maudhi si kwa Diamond tu pekee bali kwa wafuasi wake Platnumz. Mfano Alikiba anasema hatoi nyimbo kwa kukimbilia tunzo hapana, yeye hutoa nyimbo kwakufurhisha nafsi yake.


Hata hivyo Diamond hajaweza kuipata mbinu ya kuitumia kumaliza mpinzani wake, na kukitia msumari moto kidonda nipale Alikiba alivyomsainisha Ommy Dipolez kwa lebo ya Rockstar 4000. Ommy Dipolez anafahamika kuwatolewa na Alikiba kimuziki, lakini baadaye alikimbilia kuwa mwendani wa karibu wa Diamond. Urafiki ambao haukudumu kwa mda mrefu, hatua ya Dipolez kuhamia Rockstar, ilikuwa kama Korea Kusini wanavyofanya majaribio ya makombora ya nyukilia, maana Marekani roho zinawapapa. Diamond anafahamu fika, kuwa juhudi zake za kumupiku Kiba, zimeingia dosari kubwa. Maana kemia ya vipaji hivi viwili kwa pamoja huwa taabu (Alikiba na Ommy). Na ndiposa akaanza kuamua kutoa ya moyoni kwa kurap mashairi ambayo yalimugusa Kiba moja kwa moja kupitia ( Fresh Remix) na hatimae Kiba akafanya kitu ambacho hakikudhaniwa kwa kujibu kwa tweets za kejeli zilizomvunja moyo Diamond.

Ommy Dipoz| Picha| Ommy fb

Ommy Dipoz|Wakati bado Diamond bado anajipanga kujibu, Ommy Dipolez naye akalisukuma kombora la mwaka. Ambalo lilifanya Africa yote kuelekezea macho yake kwa muziki wa wa Tanzania. Kwa kipindi hicho hicho wakati Diamond bado haja sema lolote, Alikiba akaachia Kipusa, ngoma ambayo ndani ya masaa 24 ilitazamwa mara zaidi ya 500, 000. Ikawa ni bezo kwa Diamond, hivyo kuizima makali ngoma hii Diamond hangeweza akiwa pekeyake. Kwani kunangoma foleni nzima ametoa kwa mpigo ikiwemo Eneka, I miss You video nazingine ila hazikuwa zimepata mapokezi ya juu kama vibao vya awali.
Hivyo njia bora na rahisi ikawa nikuikusanya kwaya nzima ya WCB wakiwemo, Rich Mavoko, Rayvany, Harmonize, Lavalava, Queen Darlin na yeye kinara Diamond mwenyewe. Ila cha kufadhaisha ni, Ommy Dipolez akawa mwepesi kwa kuwajibu kwa tweet ya kuwakejeli. Baada ya kupost picha yenye kuonyesha Tembo akivamiwa na Simba marara na watoto wake, ila Tembo bado anasonga nikama ambaye hasikii lolote. Diamond alikuwa amefanikiawa kuivaa heshma kubwa kuliko mwanamuziki yeyote wa umri wake Tanzania, ila tamaa ya kuwaangusha na kwafanya wenzake waonekane sikitu mbele yake imemuponza. Amempa kilemba Akiba na taji la ufalme bureee. Maana yeye hashindani, ila anajiridhisha mwenyewe. Wahenga wanasema usimuamushe aliyelala, maana akiamuka utalala weye. Itabaki kuwa Alikaba anabebwa kwa kiki, huku mkisahau Diamond pia anategemea sana skendo yake na Alikiba kujikokota kwa game...kiki ni siki, mwasho ukiisha basi ladha nayo husha. Diamond arudi kwenye drawing board, na ajipange upya...maana kitumbua kimeingia mchanga.

Post a Comment

Previous Post Next Post