Katika ulimwengu wa sanaa yeyote ile, nilazima msanii au wasanii husika bayana kupitia changamoto nyingi wakati wa harakati zakutaka kufaulu. Sanaa imetumika kama silaha yenye makali ya patayo, na imekuwa nguzo muhimu kwenye jamii inayotumika haswa na wengi walio wanyonge kuwasilisha malalamiko yao kwa urahisi kwenye jamii flani. Ndiposa ikatokea dhana halisi ya msanii kuwa kio cha jamii chambilecho wimbo Darubini Kali wa mkongwe wa Bongo Flava Afande Sele alivyotangulia kuimba.


Eminem, Roma Mkatoliki na 2Pac Shakur| Photo Courtesy| Changez Ndzai
Eminem, Roma Mkatoliki na 2Pac Shakur| Photo Courtesy| Changez Ndzai
Msanii Roma Mkatoliki amekuwa kwenye uga wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama Bongo Flava kwa mda mrefu. Lakini pamoja na uzoefu wake na umaarufu wake pia, alikua hajafaulu kuufikia upeo wamafanikio yake kwenye muziki ikilinganishwa na wanamuziki wenzake wa muziki wa kufoka nchini Tanzania wakiwemo wakina Proffessor Jay, Nay Wa Mitego, Darassa, Joe Makini, Ay, FA na kadhalika. Yeye mwenyewe alishalikubali hili, wakati alipopatwa na janga la kutekwa akiwa pamoja na wenzake na kundi la watu wasio julikana. Nikimunukuu maneno aliyoyanena wakati anahojiwa na wanahabari baada ya kuapatikana. Roma alisema maneno haya '' Kunawatu wanafikiri tunatumiawa na wanasiasa kwa minaajili ya masilahi yetu. Hapana sisi niwatu wachini sana, maisha yetu ni ya kimaskini na hatuna lengo lolote baya tunaficha'' kuonyesha kuwa licha ya yeye kuwa maarufu sana, lakini alikuwa bado hajafaulu kimaisha na uchochole ulikuwa bado unamung'ata.


Roma Makatoliki Akiwa Katika Ubora Wake| Photo Courtesy| Roma fb
Roma Makatoliki Akiwa Katika Ubora Wake
Lakini kwasasa namuona Roma anachekea kicheko cha chini kwa chini hadi kwenye banki. Hii ni baada ya kutoa kibao chake kipya kwa jina #Zimbabwe, ambacho amekitumia kujibu maswali yote ambayo watu wengi walikuwa wanajiuliza baada ya kitendo kile cha kutekwa nyara kwakwe akiwa na wenzake. Nikinukuu mshororo huu katika mashairi ya wimbo huu Zimbabwe, ''Weka bunduki chini si tushindane na hoja, Sote lengo letu nikuijenga Tanzania moja '', katika mshororo huu kwenye shairi la wimbo Zimbabwe Roma amefafanua kimatiki kupitia fasihi simulizi, kuwa waliomteka hawakuwa wahuni ila watu wenye nguvu pengine serekalini.


Roma - Zimbambwe [Official Music Video]

Nikupitia ujumbe huu mkali, na wenye kuvutia ambao umeweza kuwafanya watu watabaka mbalimbali kukimblia YouTube kuitazama video ya wimbo huu mara zaidi ya 756,355…...ndani ya siku tano tangu video ipakiwe kwenye channel ya Youtube ya Roma. Rekodi ya kipekee ambayo wachambuzi wenzangu wa muziki nchini Tanzania wametangulia kusema haijawahi kutokea kuwekwa na msanii yeyote ila yeye. Roma amejitengenezea jina zaidi na kujipa nafasi ama fursa na heshima kubwa kwenye uga wa muziki wa Hip-Hop, kwani ugumu uliopo kwenye parawanja ya muziki na ushindani wake hapa Africa Mashariki umewaacha wengi wakilia na kulalama kutengwa na wadau wa muziki. Ila kwa nafasi hii Roma Mkatoliki amejikatia tikiti ya umaarufu kupindukia na milango ya Banki iko wazi si kwa kuzistiri pesa zake tu, ila kwa matumizi pia na kujiendeleza kisanaa na kimasha kama wasanii wengine waliofanikiwa Africa kupitia show na endorsements deals kutoka kwa makampuni mbalimbali ambazo zinamukodolea macho.

Kwanini Na Mfananisha Na Tupac Shakur Na Eminem?

Tupac Shakur alikuwa rapper, muigizaji na mwanaharakati wa kutetea haki za wanyonge weusi nchini Marekani. Kwa juhudi na hulka yake hiyo, mara kwa mara alijikuta akiwa upande mbaya wa sheria. Katika mwaka wa 1992, Albamu ya msanii Tupac(Tupacalypse) ilitishiwa kudenguliwa kutoka kwenye maduka ya muziki nchini Marekani, huku aliyekuwa makamu wa Raisi nchini Marekani kwa wakati huo Dan Quelye akiwa katika mstari wa mbele kupiga kampeni hiyo kwasababu yakusema nyimbo zilizokuwa katika albamu hiyo zilichangia kuawa kwa maafisa wa polisi na vijana weusi nchini Marekani. 


Rapper Na Mwanaharakati 2Pac Shakur| Photo Courtesy| 2pac fb
Rapper Na Mwanaharakati 2Pac Shakur

Jambo ambalo lilipingwa vikali na Tupac akijitetea kuwa albamu hiyo ilikuwa imebeba ujumbe wakutetea haki za wanyonge ama vijana weusi didhi ya kudhulumiwa na polisi.
Mwaka uliofatia, wa 1993 Tupac alijipata pabaya tena baada ya kudaiwa kumnajisi mwanadada ambaye Tupac kwa upande wake alijitetea kuwa mdada huyo alikuwa yuko kwenye mahusiano naye. Hivyo hakumubaka kama taarifa ya polisi ilivyokuwa ikidai. 

Rapper Na Mwanaharakati 2Pac Shakur| Photo Courtesy| 2Pac fb

Kesi ambayo jaji alimpata na hatia msanii huyo naikamfanya Tupac ahukumiwe jela kwa kifungo cha mwaka mmoja gerezani lakini akaponea nje kwa bondi. Lakini hata hivyo miaka mitatu baadaye, ndani ya mwaka wa 1993 alijipata mashakani tena kuhusiana na kesi hiyo kwani jaji alidai masanii huyo alikwenda kinyume na maagizo ya koti hivyo akapigwa faini ya kifungo cha siku mia moja ishirinigerezani ama kutozwa bondi. Mbali na shida alizozipata Tupac Shakur kwasababu ya msimamo wake wakutetea waamerika weusi wenzake haswa vijana, lakini pia aliibuka kuwa masanii maarufu na tajiri zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani kwa wakati huo huku akiuza zaidi ya kopi milioni 75 za albamu zake duniani kote.

Rapper Na Muigizaji wa Filamu Eminem| Photo Courtesy| Fb
Rapper Na Muigizaji wa Filamu Eminem Katika ubora Wake
Star wengine wa Marekani aliyepitia mambo kama ya Roma Mkatoliki ni Eminem. Alizaliwa kama Martial Bruce Mathers III, lakini kwajina la ulingoni mwa sanaa anafahamika kwa jina maarufu kama Eminem. Msanii huyu ambaye ameweka rekodi tofauti tofauti kwenye sanaa ya muziki wa Hip-Hop duniani, ameshawahi kijikuta kwenye mkono mbaya wa sheria mara si haba. Mwaka wa 1999, mamake mzazi ambaye anafahamika kama Debora Nelson Mathers, alimushataki nyota huyo wa Hip-Hop kwa madai kuwa ujumbe uliokuwa kwenye wimbo wake wa ''Slim Shade LP'' ulikuwa unamuhusu yeye.
Eminem Akiwa Kwenye Pozi Lake| Photo Courtesy| facebook
Eminem Akiwa Kwenye Pozi Lake
Kwahivyo ulimukera na akamushtaki na kukwamilia kulipwa na mwanwe kiasi cha Dolla za kimarekani US$ milioni 10. Lakini hatahinyo licha ya Eminem kupatikana na hatiya, mamake mzazi aliambulia kuvuna kiasi cha Dolla za Kiamrekani US $ 1,600 pekee ndani ya mwa wa 2001. Kesi hii na nyingine mbalimbali ambazo ziliwahi kumwanda nyota huyu, zilimuacha na mafanikio makubwa ikiwamo umaarufu na utajiri huku ikitajwa msanii aliye uza albamu kopi milioni 12.1 katika mwaka wa 2000. Kwahivyo kupitia hatua na changamoto za Tupac na Eminem, inaonyesha wazi kuwa Roma anadalili za kusifata nyayo za mastaa hawa na tayari angeichukua fursa hii ambayo imemukujia kujitengenezea kesho yake iliyo njema na inayong'ra kwani tayari madali ya endorsements kudoka kwa makapuni na shows kibao zinamkodolea macho staa huyu wa Hip- Hop.

Post a Comment

Previous Post Next Post