Ukarabati wa uga wa Rostov wanoga kwa maandalizi ya kombe la dunia mwakani
Uga wa Rostov Arena, Urusi ukikarabatiwa sehemu ya paa. Picha/Kwa hisani
Uga wenye uwezo wa kuingiza mashabiki wapatao  45,000 unakarabatiwa kusini mwa taifa la Urusi kwa maandalizi ya kipute cha kombe la dunia mwaka wa 2018.

Uga huo kwa jina Rostov Arena utakaoandaa mechi nne za makundi sawa na mchuano wa raundi ya 16 upo katika upande wa kushoto wa Don Rover.


Gavana wa eneo la Vasily Golubev, amesema ukarabati wa uwanja huo kwa sasa umefikia asilimia 85 na 86  na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba mwaka huu. 

Baada ya michuano hiyo ya kombe la dunia, uwanja huo utatumika kama makao ya klabu ya Urusi iitwayo Rostov katika kuandaa mechi zake za nyumbani.

Post a Comment

Previous Post Next Post