Timu ya Ulinzi ya Handiboli ikinyanyua kenya na medali ilizoshinda kwenye makala ya 10 (2016) ya ubingwa wa majeshi kanda ya Afrika mashariki. Picha?Kwa hisani
Timu ya Ulinzi ya Handiboli ikinyanyua kenya na medali ilizoshinda kwenye makala ya 10 (2016) ya ubingwa wa majeshi kanda ya Afrika mashariki. Picha?Kwa hisani
Mabingwa mara nne wa ligi kuu soka taifa Kenya (KPL), Ulinzi Stars wataondoka nchini kuelekea Bujumbura, Burundi kushiriki makala ya mwaka huu ya mashindano ya majeshi, kanda ya Afrika Mashariki.
Makala hayo ya 11 ya mashindano na utamaduni yatang’oa nanga mnamo Agosti 24 na kutamatika Septemba 8 huku kikosi cha ulinzi cha Kenya (KDF) kikituma ujumbe wa watu 121 wakijumuishwa washiriki na maafisa wasimamizi.
Jiji kuu la Burundi litaandaa timu kutoka Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda pamoja na wao ambapo zitaonyeshana ubabe katika fani tofauti za michezo ikiwemo soka, handiboli na netiboli.
KDF iliibuka mshindi wa ujumla katika makala yaliyopita yaliyoandaliwa nchini Rwanda baada ya kunyakua nishani ya dhahabu katika fani tatu kati ya tano za michezo.
Matokeo yao bora yalikuwa katika mchezo wa handiboli pamoja na mbio za nyika.
Mwaka jana Ulinzi ilishinda taji la soka baada ya wenyeji Rwanda kushindwa kufunga zaidi ya bao moja kwenye mechi dhidi ya Tanzania na hivyo kutawazwa mabingwa.
Katika ligi kuu soka nchini, mabingwa hao wa mwaka wa 2010 walirejelea mfumo wa ushindi kwa kuichuna Chemilil Sugar goli 1-0 lililopachikwa wavuni na Daniel Waweru uwanjani Afraha mnamo Jumanne ya Agosti 22, ni ushindi uliowapa motisha wanapojiandaa kushiriki ubingwa wa majeshi.
Mashindano hayo ya majeshi yatafunguliwa na kufungwa rasmi katika uwanja wa taifa wa Prince Louis Rwagasore.
Kinyang’anyiro hicho kilicho na nembo ‘One People One Destiny through EAC Military Games and Cultural Event 2017’ kitahusisha zaidi ya washiriki 500 watakaowakilisha vikosi mbali mbali vya ulinzi katika jumuia ya Afrika mashariki.Post a Comment

Previous Post Next Post