Wanaoska wa Ulinzi Stars wakisherehekea ushindi dhidi ya Al Hilal kwenye mechi ya  kombe la CAF Confederation uwanjani Safaricom stadium Kasarani,  February 18, 2017. Ulinzi Stars FC walishinda kwa mabao 5-4 ya penanti. Photo/Stafford Ondego/www.sportpicha.com
Wanaoska wa Ulinzi Stars wakisherehekea ushindi dhidi ya Al Hilal kwenye mechi ya  kombe la CAF Confederation uwanjani Safaricom stadium Kasarani,  February 18, 2017. Ulinzi Stars FC walishinda kwa mabao 5-4 ya penanti. Photo/Stafford Ondego/www.sportpicha.com

Klabu ya Ulinzi Stars imekwea alama nafasi moja hadi ya nne kwenye jedwali la ligi kuu soka taifa Kenya KPL, hii ni baada ya kunusuru ushindi finyu wa goli 1-0 dhidi ya Chemilil Sugar katika mechi iliyopigwa adhuhuri ya Agosti 22 ugani Afraha Nakuru.

Goli hilo la pekee lilisukumwa kimiani na Daniel Waweru kunako kipindi cha kwanza cha ngoma hiyo kupitia mkwaju wa tuta.

Chemilil,ukipenda waite wakata pingili za miwa, walishinda mkondo wa kwanza kwa magoli 2-1 ambapo Jefari Odeny na Victor Majid aliyetokomea AFC Leopards walikiramba kimia huku Ulinzi wakifutwa machozi na Oscar Wamalwa aliyeunganisha wavuni penanti ya dakika za lala salama.

Chemilil hadi sasa hawajashinda katika mechi saba zilizopita huku ushindi wao wa mwisho ukijiri mwezi juni katika uchanjaa wa Chemilil Complex mikononi mwa viana wapya ligini Nzoia Sugar FC, na huenda wakajipata pabaya zaidi endapo Nakumatt, Mathare United, Afc Leopards na Sony Sugar zitasajili ushindi katika mechi zao mtawalia wiki hii.

Ulinzi wana kibarua dhidi ya Gor Mahia katika mchezo ujao huku Chemilil wakitarajia kumaliza mkosi wa kudondosha alama watakapokuwa wenyeji wa Muhoroni Youth waliosagwa 2-1 na Gor wikendi jana ugani Kisumu.

Ushindi wa hapo jana kwa Ulizi licha ya kuwaacha katika nafasi ya 4 kwa alama 32 baada ya ushiriki wa mechi 20, pia umewapa nguvu na msukumo wanapojipanga kuelekea nchini Burundi ili kutetea ubingwa wao wa mashindano ya Afrika mashariki baina ya majeshi.

Post a Comment

Previous Post Next Post