Roberto Firmino (kushoto) akisherehekea goli na mwenzake Jordan Henderson kwenye mechi ya raundi ya mchujo wa UEFA Champions League dhidi ya Hoffenheim tarehe 23/08/2017. Liverpool walishinda kwa mabao 4-2. Picha/Getty Images

Nafasi 10 za mwisho za kuingia hatua ya makundi ya ligi ya mbingwa barani Uropa zilijazwa zote hapo jana baada ya timu tano za mwisho kupatikana kutoka kwenye raundi ya mchujo na miongoni mwao ikiwa Liverpool waliyoinyoa Hoffenheim ya Ujerumani mabao 4-2 ugani Anfield.
Liverpool wamesonga kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya kushinda 2-1 mechi ya kwanza nchini Ujerumani  wiki iliyopita.
Mabao yao hapo jana yalifungwa na Emre Can, dakika ya 10, Mohammed Salah dakika ya 18 na Roberto Firmino dakika ya 63 wakati Hoffenheim wakifungiwa na Mark Uth, dakika ya 28, na Sandro Wagner dakika ya 79.
Pamoja na Liverpool, timu nyingine zilizofuzu kuingia makundi hapo jana ni Apoel, Cska Moskva, Qarabag na Sporting.
Timu nyingine tano zilizofuzu juzi ni Celtic, Olympiakos piraeous, Maribor, Sevilla na Napoli.
Droo ya kupanga makundi ya mashindano hayo itafanyika hii leo leo saa moja usiku kwenye ukumbi wa Grimaldi Forum, Monaco na Uingereza itakuwa na timu 6 kwenye vyungu vya droo.
Post a Comment

Previous Post Next Post