David 'Cheche' Ochieng (kushoto) akiwa mazoezini na wenzake wa timu ya taifa. Picha/Stafford Ondego.www.sportpicha.co.ke
David 'Cheche' Ochieng (kushoto) akiwa mazoezini na wenzake wa timu ya taifa. Picha/Stafford Ondego.www.sportpicha.co.ke
Mlinzi  David ‘Cheche’ Ochieng’ amekiri kuwa kama timu ya taifa Harambee Stars, watamkosa sana nahodha Victor Wanyama watakapopambana na Msumbiji Jumamosi hii jijini Maputo.


Cheche anayepiga soka la malipo nchini Marekani, vile vile alishikilia kuwa kukosekana kwa Wanyama kutawapa changamoto wachezaji hao kudhihirisha uwezo wao katika mawindo ya kufuzu kwa kombe la mataifa bingwa Afrika mwaka wa 2019.


Klabu ya Tottenham Hotspur anamochezea Wanyama iliomba kiungo huyo anayepata afueni kutokana na jeraha asipangwe kwenye kikosi cha taifa kwa ajili ya mechi za kirafiki. 


Ni nafasi nyingine nzuri kwa mchezaji mwengine tukiendelea kumsubiri nahodha wetu Wanyama kwenye mechi ijayo.


Ni muhimu tushinde mechi yetu na msumbiji kwa kuwa itatupa ujasiri tunapojiandaa kucheza mechi za kufuzu kwa kombe la bara Afrika mwaka wa 2019. Alisema beki huyo anayecheza soka lake kaskazini mwa Marekani, ligi ya (NASL) na New York  Cosmos.


Cheche ni mwanasoka wa kigeni pekee aliyeripoti kambini huku wengine kama Michael Olunga, Ayub Timbe na Johanna ‘Tosh’ Omollo wakijiunga na Wanyama kudai kuondolewa timuni kwa sababu mbali mbali. 


Olunga amehusishwa sana na na uhamisho wa kimkopo kwenye klabu shiriki ya ligi kuu Uhispania La Liga, Girona  na huenda akawa katika harakati za kukamilisha dili hiyo baada ya kukalishwa benchi katika klabu alimokuwa ya Guizhou Zhicheng inayocheza ligi kuu Uchina.
Mshambuli wa Harambee Stars Michael Olunga, akisherehekea goli la kwanza kwenye mechi dhidi ya Zambia. Picha/ Daily Nation
Mshambuli wa Harambee Stars Michael Olunga, akisherehekea goli la kwanza kwenye mechi dhidi ya Zambia. Picha/ Daily Nation
Kwa upande wake, Tosh aliomba apewe muda wa kutulia katika klabu yake mpya ya Ubelgiji ijulikanayo kama Cercle Brugge K.S.V.


Wachezai wengine wanaopiga soka la ulaya waliwasili usiku wa kumkia leo  na watajiunga na kikosi hicho shiriki cha michuano ya kufuzu kwa AFCON kilicho kambini kwenye uga wa Kenya School of Monetary Studies (KSMS), muda mchache tu kabla ya kuondoka hapo kesho kuelekea Msumbiji.

Kocha mkuu wa Stars Stanley Okumbi amewaita wachezaji 54 timuni ila akasema timu hiyo imegawanywa mara mbili, ile itakayocheza kipute cha CHAN mwakani, na ile itakayopiga michuano ya kufuzu kwa AFCON 2019.


Kikosi cha CHAN kiliondoka jana ambapo kinatarajiwa kucheza na Mauritania na Morocco mnamo Agosti 31 na Septemna tarehe 4 mtawalia.

Okumbi anaamini kutokana na mabadiliko machache timuni, kikosi chake kitakuwa dhabiti na kuandikisha matokeo ya kufana.
Wachezaji wengi watakaopambana na Msumbiji ni wale wale waliocheza kwenye mechi zingine zilizopita za kirafiki.
Timu iliyo Morocco ni yetu ya CHAN na tunafaa kujiandaa kwa hilo pia. Alidai Okumbi.
Okumbi aidha alisema idadi kubwa ya wanasoka wa kigeni wanaokosa kwenye kambi yake ya mazoezi imeathiri mipango yake ya kukikita kikosi ila akatetea uamuzi wa kumpuuza beki shoto Eric ‘Marcelo’ Ouma anayechezea nchini Georgian na klabu shiriki ya ligi kuu, FC Kolkheti.
Mara ya mwisho tulipokuwa tukipambana na Sierra Leone nilichakatua mchezo wa Marcelo na hakuwa na mvuto vile, si Marcelo niliyemfahamu akiwa Gor Mahia.
Eric 'Marcelo' Ouma kwenye mechi ya kufuzu kwa AFCON dhidi ya Congo. Picha/Enos Teche
Eric 'Marcelo' Ouma kwenye mechi ya kufuzu kwa AFCON dhidi ya Congo. Picha/Enos Teche 
 Naweza kusema ligi yao haina viwango. Tunapomwacha nje ya kibarua hiki najua atafanya bidii zaidi ili ajumishwe timuni wakati mwengine. Aliweka sawa Okumbi.
Kuhusiana na kipute cha kufuzu kwa AFCON, Okumbi alisema atazingatia sana kuchonga safu ya ulinzi na ile ya kumalizia.


Post a Comment

Previous Post Next Post