Rapper mkali wa Bongo Flava maarufu kama Chidi Benzi, amezua lipya Alhamisi hii ya leo baada ya kutoa kauli moja ambayo imezua utata. Chidi Benzi ambaye anafahamika kwa kipaji chake kikali cha kuchana, na ameshawahi kuiwakilisha nchi ya Tanzania vyema kama msanii au rapper. Hivi karibuni Chidi Benzi amehusishwa na kashfa za utumiaji wa madawa ya kulevya, hatua ambayo ilipelekea yeye kupelekwa sober house kwaajili yakupata huduma za urejeshaji wa hali yake ya kawaida. Ila katika interview ambayo amefanyiwa na channel ya EastAfricaTV kwenye kipindi cha ENEWZ, Chidi amekana kutumia mihadarati na wanao sema hivyo hawana nia njema ila kumuharibia jina tu. Mbali na hivyo Chidi amewashangaza wengi Bongo, baada yakusema huwa anaongea na marehemu Tupac Shakur kwanjia ya simu. Nakutokana na hivyo, anapanga kumrudisha kwenye game na anampago wakumuleta Bongo kwaajili ya uinduzi wa collabo yao hao wawili.

Chidi: Halafu ulikua unanihoji nini kuhusu simu?

ENEWZ: Nani ulikua unaongea naye kwenye simu, naonamazungumuzo yamekuamengi

Chidi: Nilikua naongea na Tupac

ENEWZ: Ulikua unaongea nanani?

Chidi: Tupac, Tupac Omary Shakur

ENEWEZ: Tupac wa Manzeze ama Tupac wa mabibo....

Chidi: Tupac yule unaemujua, si wamanzeze ama wabibo, wamabibo siunajua ni Tupac wa kitupac


Kwa uhondo kamili hebu tazama kiambatanisho hiki cha YouTube ili upate burudani kamili.Post a Comment

Previous Post Next Post