Ndani ya wiki moja iliyopita kumekua na drama ndani ya muziki wa Bongo Flava, ambapo msanii na nguli wa muziki Tanzania Diamond Platnumz alishirikishwa kwenye ngoma ama Refix ya wimbo (Fresh) wa mkongwe Farid Kubanda a.k.a Fid Q. Diamond alichukua hatua ama fursa ile kumchana moja kwa moja mkali wa Aje Alikiba, ambaye kwa upande wake aliichukulia kuwa kejili na kujibu kwa tweet iliyozua tafrashani si haba kwenye mitandao ya kijamii. Huku makundi mawili hasimu ya mitandaoni maarufu team Kiba na team Diamond,yakionekana kung'atuana vikali hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa. Hata hivyo, baada ya mapambano hayo kwenye mitandao ya kijamii. Alikiba alichukua fursa hiyo kuachia kibao chake kipya kwa jina Seduce Me, ambacho kilifatiwa na kibao cha kundi zima la WCB kwa jina zilizopendwa. Mapambano yakawa bado yanaendelea, ila Alikiba ameonekana kupata mafanikio zaidi ya mwenzake, kwaani mastaa wengi nchini Tanzania hata wa muziki wa njili akiwemo Christine Shusho, kujitokeza na kumsifia Alikiba kwa kazi yake hii mpya na mrua.


Fredrick Bundala| Picha na| Fredrick Bundala fb
Mtangazaji Na Muandishi Dr. Fredrick Bundala

Na nikufatia mkulupuko huu, nimeamua kukusogezea simulizi, ambazo zimekuwa zikichambua hali hii yote tokea mwanzo hadi sasa pale imefikia. Dr. Fredrick Bundala, ni mwandishi na mtangazji wa habari nchini Tanzania. Na anauzoefu wa hali ya juu ikifika na mambo ya changanuzi ya mambo ya brudani. Amekuwa katika mstari wa mbele katika hali ya kuwakuza wasanii mbali mbali nchini Tanzania ikiwemo Alikiba na Diamond. Hivyo sikwamba yupo pale  anabahatisha, hapana, ila anafahamu hali halisia ya wasanii hawa wawili kabla na baada ya kuupata umaarufu. Hapa amekuwa mwepesi kuangazia maajabu ama mafanikio ya mda mfupi yaliyotokana na nyimbo hii Seduce Me yake Alikiba. Ambayo imevunja na kuweka rekodi mpya kabisa katika muziki wa kizazi kipya Africa Mashariki. Pia leo tu AFRIMMA wametangaza majina ya wasanii teule kote Africa ambao wanang'anga'nia tuzo mbalimbali kwenye vipengele tofauti za tunzo hizo. Na tayari imebainika wanamziki zaidi ya wanane kutoka Tanzania wametajwa kwenye orodha ile huku Alikiba akiongoza orodha ya Watanzania hao kwa kutajwa kwenye vipengele vinne tofauti na wimbo wake Aje. Hebu fatilia simulizi hizi hapa kwa uhondo kamili. Burudika!

Post a Comment

Previous Post Next Post