Elijah Manangoi baada ya kushinda dhahabu ya mita 1500 kwenye ubingwa wa riadha duniani jijini London mnamo Agotsi, 13. Picha/Getty Images
Elijah Manangoi baada ya kushinda dhahabu ya mita 1500 kwenye ubingwa wa riadha duniani jijini London mnamo Agotsi, 13. Picha/Getty Images
Wanariadha wa Kenya watafukuzia ubingwa kwenye mashindano ya IAAF Diamond League jijini Zurich hii leo.
Huku akivuna ushindi wa kufana katika mikondo ya Doha na Monaco, bingwa wa dunia Elijah Manangoi atawaongoza wenzake katika usasi wa ushindi wa mbio za mita 1500.
Mwenzake mazoezini Timothy Cheruiyot, aliyenyofoka na medali ya fedha katika mashindano ya London mbele ya Mnorway Filip Ingebrigtsen, pia atakuwa katika mchakato wa kufukuzia ushindi kwenye mbio hizo zitakazotimkwa katika mji mkuu nchini uswizi.
Mwengine kinyanga’nyironi atakuwepo mshindi wa nishani ya dhahabu jijini Beijing wakati wa mashindano ya olimpiki na mshindi mara tatu wa dunia Asbel Kiprop aliyeshinda taji hilo mara tatu.

Asbel Kiprop aliponusia kuvunja rekodi ya ulimwengu ya mita 1500 jijini Monaco mnamo 18/7/2015. Picha/Getty Images
Asbel Kiprop aliponusia kuvunja rekodi ya ulimwengu ya mita 1500 jijini Monaco mnamo 18/7/2015. Picha/Getty Images
Upinzani mkali aidha unatarajiwa baina ya Manangoi na Cheruiyot huku wote wakinakili rekodi za muda bora duniani msimu huu.
Katika mwanzo wa Diaond League jijini Doha, Manangoi aliandikisha muda wa dakika 3:31.90 kabla ya Cheruiyot kuushusha jijini  Stockholm kwa dkaika 3:30.77.
Manangoi atapambana kuuteka tena uongozi wa ulimwengu jijini Monaco kwa muda wake bora maishani wa dakika 3:28.80, wiki mbili kabla ya kutwaa dhahabu katika ubingwa IAAF jijini London.
Katika masafa ya mita 3000 urukaji vizuizi na maji, wanariadha wa Kenya watajaribu kuzima upinzani kutoka kwa Emma Coburn, aliyeongoza mmarekani mwenzake kutawala nafasi mbili za kwanza katika ubingwa wa dunia yapata wiki mbili zilizopita.
Mshindi wa nishani ya fedha kwenye mashindano ya olimpiki jijini Rio na bingwa wa dunia jijini Beijing Hyvin Kiyeng, atamwongoza bingwa wa jumuia ya maodla Purity Kirui na bingwa chipukizi wa ulimwengu Celliphine Chepteek Chespol miongoni mwa wanariadha wengine, licha ya kuzalisha matokeo duni jijini London.
Kiyeng aliachia ubingwa wake mjini Corbon na kuridhika na shaba huku Beatrice Chepkoech, Chespol na Purity Kirui wakimaliza katika nafasi za nne,sita na 10 mtawali.
Mshindi wa shaba jiini Rio Margaret Nyairera atatarajia kutamba kwenye masafa ya wake ya mita 800, hii ni baada ya kumaliza wa nne jijini London huku bingwa wa ulimwengu jijini Moscow mwaka wa 2013 Eunice Sum, aliyerejelea hali yake ya kawaida, akijiunga na Nyairera katika mawindo ya dhahabu kwenye masafa hayo ya mita 800.
Sum, alijiondoa nje ya ubingwa wa dunia baada ya kuwa mgonjwa jioni ya siku ya kuanza ya mashindano na upinzai wao mkubwa utatoka kwa Mafrika kusini na bingwa mara tatu wa dunia Caster Semenya.
Semenya, anayepigiwa upato mkubwa kung’ara kwenye masafa hayo, atatarajia kutetea taji la Diamond League katika maasa ya mita 800 ila atakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Mburundi Francine Niyonsaba aliye na nishani mbili za fedha kutoka kwa mashindano ya olimpiki jiini Rio na yale yaliyokamilia si kitambo ya dunia pamoja na Wambui.
Mwanariadha wa Afrika kusini Caster Semenya akisherehekea ushindi wake wa mita 800 kwa wake, jijini London kwenye ubingwa wa dunia  mnamo13/8/2017. Picha/Getty Images
Mwanariadha wa Afrika kusini Caster Semenya akisherehekea ushindi wake wa mita 800 kwa wake, jijini London kwenye ubingwa wa dunia  mnamo13/8/2017. Picha/Getty Images
Masafa ya 5000 kwa wanaume yataibua upinzani si haba ambapo bingwa mara nne wa olimpiki na bingwa mara sita wa dunia Mo Farah, atakapokutana na Methiopia Muktar Edris baada ya kumnyima ubingwa wa dunia katika udongo wa nyumbani yaani nchini Uingereza siku 10 zilizopita.
Mo atakuwa anashindana kwa mara ya mwisho kwenye mbio huku mshindi wa mwaka jana wa fedha ambaye ni mzawa wa Kenya japo raia wa Marekani Paul Chelimo, akinenwa pia kuwa na uwezekano wa kushinda mtimko huo pamoja na mshindi wa zamani wa nishani ya shaba kwenye mashindano ya Afrika Ronald Kwemoi, na pia Cornelius Kagogo.
Jumla ya kitita cha dola laki moja za kimarekani sawa na shilingi milioni 10.32 za Kenya kitashindaniwa katika fani 16 za ubingwa huo wa Diamond League mikondo yote, ya Zurich na Brussels na jumla ya zawadi mseto ya (Ksh 330.240M) na (Ksh 5.16M) pamoja na kombe la Almasi kwa kila mshindi.Tunu ya pesa taslimu ni kama ifuatavyo… 
Mshindi wa kwanza – US$ 50,000  (Ksh 5.16M)
Mshindi wa pili – US$ 20,000 (Ksh 2.064M)
Mshindi wa tatu – US$ 10,000 (Ksh 1.032M)
Mshindi wa nne – US$ 6000 (Ksh 619,200)
Mshindi wa tano – US$ 5000 (Ksh 516,000)
Mshindi wa sita – US$ 4000 ( Ksh 412,800)
Mshindi wa saba – US$ 3000 (Ksh 309,600)
Mshindi wa nane – US$ 2000 (Ksh 206400)


Post a Comment

Previous Post Next Post