Mshindi wa medali ya dhahabu Nick Okoth akiwa mazoezini,Picha kwa hisani ya Standard Digital
Mshindi wa medali ya dhahabu Nick Okoth akiwa mazoezini,Picha kwa hisani ya Standard Digital
Kikosi cha Kenya cha wanandondi watatu kilichoondoka kilichosafiri kuwakilisha taifa kwenye mashindano ya kimataifa ya AIBA – 2017 jijini Hamburg, Ujerumani kimerambishwa sakafu kwenye awamu ya makundi.
Nick Okoth, John Kyalo na Shaffi Bakari ambao waliokabidhiwa bendera ya taifa na Shirikisho la mchezo wa ndondi nchini (BAK) kuipeperusha wakati wa mashindano hayo ya kimataifa, wamewewesuka na  kuuramba mchanga.

Wa kwanza kupoteza alikuwa John Kyalo ambaye alivurugwa kwenye mechi yake na mwingereza Benjamin Whittaker kwa pointi 5-0 katika uzani wa (Middle weight) siku ya kwanza tu ya mashindano hayo ambayo yalianza  Ijumaa.
Wa pili alikuwa ni mshindi wa nishani ya dhahabu kwenye mashindano ya Afrika yaliyofanyika nchini Congo, Nick Okoth.Okoth alidondosha alama kwa raia wa Brazil Wanderson de Oliveira 5-0 kwenye uzani wa (Lightweight).

Baada ya wawili hao kupoteza mapigano yao, matumaini ya wakenya yalisalia kwa Shafi Bakari, baada ya mwanandondi huyo kutia bidii kwenye pigani la kwanza, hali iliyompa fursa ya kushiriki pigano la pili la makundi kabla ya awamu ya muondoano.

Hata hivyo mgema akisifiwa tembo hulitia maji, Bakari alisasambuliwa kwenye mechi ya pili na Mjerumani Omar Ibrahim Saleh wikendi iliyopita kwa alama 5-0 kwenye uzani wa (Middleweight) na kuyayeyusha matumaini ya Kenya kuwa na mwakilishi kwenye mashindano hayo yanayoendelea kwa sasa.

Akizungumza na meza yetu ya michezo, kocha wa kikosi hicho David Munuhe alihoji kuwa ushindi wa Bakari ulipewa hasimu wake na refa wa mchezo.
Huu ulikua mchezo wa pekee kwetu na haswa kwa Bakari mwenyewe alilifahamu hilo na alitia bidii kwenye awamu zote tatu za mchezo, ila nashangaa kuona kuwa ushindi wake umepewa mtu mwingine. Alilalamika Munuhe.
Michezo yote ya awamu ya makundi ilikamilika jana Agosti 28 huku mataifa 31 yakitinga awamu ya muondoano .

Maelezo zaidi kutoka kwa Simon Ngaira

Post a Comment

Previous Post Next Post