Kieran Gibbs wa Arsenal. Picha/Getty Images
Kieran Gibbs wa Arsenal. Picha/Getty Images
West Brom wanakaribia kukamilisha ununuzi wa beki wa kushoto wa Arsenal Kieran Gibbs.


Klabu hizo mbili zimeafikiana ada ya £5m kwa mchezaji huyo wa miaka 27 ambaye pia alikuwa akifanya mashauriano na Watford pamoja na klabu ya Galatasaray ya uturuki.

Gibbs bado atahitajika kufanyiwa uchunguzi wa matibabu kabla ya kutia saini mkataba wake.Kwingineko, Arsenal wamejiunga na Manchester City na Leicester City katika kutaka kumsajili beki wa kati wa West Brom Jonny Evans.

Evans ataruhusiwa kuondoka Hawthorns iwapo tu West brom watafanikiwa kupata mchezaji wa kujaza pengo atakaloacha.


Wanamtaka zaidi mchezaji wa Manchester City Eliaquim Mangala na iwapo Manchester City watamtaka kwa kweli Evans, basi uhamisho huo utakuwa rahisi.


Post a Comment

Previous Post Next Post