Wachezaji wa Barding wakisherehekea baada ya kufunga goli dhidi ya Passenga kwenye nusu fainali ya dimba la Airtel Rising Starsmjini Kisumu. Picha/Kwa hisani
Wachezaji wa Barding wakisherehekea baada ya kufunga goli dhidi ya Passenga kwenye nusu fainali ya dimba la Airtel Rising Stars mjini Kisumu. Picha/Kwa hisani


SOKA

Wawakilishi wa Kenya kwenye soka ya akina dada katika ubingwa wa Afrika Mashariki baina ya shule za upili (FEASSSA) unaonendelea mjini Gulu Uganda Wiyeta Girls watamenyana na Basile ya Burundi katika hatua ya robo fainali.

Wawakilishi wengine wa taifa hili kwenye fani hiyo Ibinzo itakuwa na kibarua cha ziada katika hatua hiyo kwani imepangw akukutana na Alliance ya Tanzania  huku Kawempe ikisakatana na Mutunda ya Rwanda.Robo fainali ya mwisho itashuhudia Uganda Martyr’s Rubaga ikishikana shati na Mukono High.VIKAPU

Hapo jana kwenye siku ya 4 ya mashindano, mabingwa wa taifa Upper Hill walilishwa vikapu  68-78 na PS Baptiste ya Rwanda katika mpira wa vikapu. Laiser Hill walipoteza seti ya kwanza kwa 10-12, kabla ya kuteleza tena kwa vikapu 17-09 kwenye seti ya pili. 

Katika seti ya tatu walipoteza kwa seti 23-26 kabla ya kushinda seti ya pekee kwa vikapu 26-23.
Katika vikapu kwa akina dada Kaya Tiwi ililimwa 47-37  na Buddo ya Uganda huku Togoi ikipoteza 59-48 mikononi mwa Ldk ya Rwanda.
VOLIBOLI

Malava iliwanyamazisha Buremba seti 3-1 za 25-20, 18-25, 25-18 na 27-25.Cheptil iliwakaranga Namugongo ya Uganda seti 3-0 za 25-16, 25-12 na 25-20 huku Kwanthanze ya Kenya ikiwanyeshea St Brigids ya Uganda  seti 3-0 za 25-06, 25-22 na 25-07.


Post a Comment

Previous Post Next Post